ADAI BARNABA HANA KITU, HAWEZI KUMTOZA KWA VIDEO ALIYOMSHIRIKISHA WIMBO ‘MAGUBEGUBE’
![]() |
Mpoki (wa pili kulia) akiwa na wasanii wenzake wa kundi la Orijino Comedy. |
Mpoki (kulia) akiwa na nyota wa bongoflvea, Barnaba. |
Na Sanula Athanas
Msanii nyota wa vichekesho
nchini, Sylivester Mjuni ‘Mpoki’, amesema kuwa yeye hujiingizia fedha nyingi
kupitia fani yake na hivyo hana sababu ya kumtoza hela msanii yeyote wa muziki
wa bongofleva anayetaka kushirikiana naye kurekodi nyimbo zake.
“Nimekuwa nikishirikishwa na
wasanii wengi tu wa ‘Bongo’ lakini siwatozi chochote maana hawana mshiko wa
kutosha, leo nimwambie Barnaba anilipe Sh. Milioni 50 kutokana na ushiriki
wangu kwenye wimbo wake wa ‘Magubegube’ nitakuwa ninamkomoa, siku zote
nashirikiana nao ili kuwainua, kama kuna msanii amenilipa pesa aje hapa,”
amejigamba Mpoki.
“Situngi nyimbo kwa nia ya
kujipatia pesa bali nafanya hivyo ili kuburudisha mashabiki wangu. Mimi nina
kazi yangu nzuri ambayo mnaijua, inaniingizia pesa nyingi, hivyo ni kheri
nikatenga kiasi kidogo ninachokipata kutokana na kazi hiyo kuingia studio na
kurekodi nyimbo kuwaburudisha watu,” amesema Mpoki.
Wakati wasanii nchini
wakiumiza vichwa vyao kutunga nyimbo ili kujipatia fedha, Mpoki ametoa mpya
baada ya kueleza kuwa hatungi nyimbo kwa kusaka pesa bali kufurahisha mashabiki
wake.
Mpoki ameyasema yote hayo jana
asubuhi wakati akihojiwa na watangazaji wa kipndi cha ‘Leo Tena’ kinachorushwa
na kituo cha redio ya Clouds FM na kutambulisha wimbo wake mpya alioupa jina la
‘Mademu wa Kibongo’.
Msanii huyo wa kundi la
Orijino Comedy, amesema halipwi chochote na wasanii kutoka nchini ambao
wamekuwa wakimshirikisha kwenye nyimbo zao kwa kuwa kipato chao kiko chini.
Katika wimbo huo, Mpoki
anayesifika kwa misemo mikali na ya kuchekesha, anaeleza sifa za wanawake
wanaoishi katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Awali mtayarishaji wake, Lamar
ambaye alikuwa ameambatana naye, aliweka wazi juu ya usumbufu anaopata katika
kuandaa nyimbo za Mpoki, akisema kwamba ni mtu wa kuchekesha kila mahala kiasi
kwamba hata waingiapo studio, wakati mwingine hujikuta wakiishia kucheka tu badala
ya kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment