|
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye akimsisitiza jambo refa Martin Saanya mara baada ya kumkabidhi tuzo pamoja na kitita cha Sh.Milioni 3.8 ya mwamuzi bora wa ligi kuu ya Vodacom 2011/2012. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa. |
|
Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (kushoto) na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kutoa tuzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom. |
NAHODHA
wa Taifa Stars, Juma Kaseja na msaidizi wake Aggrey Morris wameng’ara
katika hafla ya kampuni ya Vodacom kukabidhi zawadi kwa wachezaji,
klabu, waamuzi na makocha waliofanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Vodacom
msimu wa 2011/2012.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika jana usiku (Juni 30 mwaka huu) hoteli ya Double
Tree Hilton, Dar es Salaam, Morris anayechezea Azam aliibuka mchezaji
bora wa ligi hiyo wakati Kaseja anayedakia Simba alikuwa kipa bora.
Kila
mmoja alizawadiwa Sh. 3,312,500 katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi
alikuwa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye. Kaseja aliwashinda makipa
Mwadili Ally (Azam) na Deogratias Munishi (Mtibwa Sugar) wakati Morris
aliwashinda Haruna Niyonzima (Yanga) na Haruna Moshi (Simba).
|
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye katikati akishuhudia Mbunge wa Tabora mjini ambaye ni Mwenyekiti wa Simba Sports Club, Aden Rage akipongezwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Vodacom, Kelvin Twisa mara baada ya kupokea tuzo ya golikipa bora wa mwaka kwa niaba ya Juma Kaseja, wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom. |
|
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye katikati akishuhudia Mwenyekiti wa Azam FC, Mohamed Said akipongezwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Vodacom, Kelvin Twisa mara baada ya kupokea tuzo ya mfungaji bora na timu yenye nidhamu na kocha bora kwa niaba ya klabu yake wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar e Salaam. |
John
Bocco wa Azam aliyefunga mabao 19 ndiye mfungaji bora, refa bora ni
Martin Saanya kutoka Morogoro ambaye aliwashinda Oden Mbaga (Dar es
Salaam) na Amon Paul (Mara) wakati kocha bora ni Stewart Hall wa Azam
aliyewashinda Charles Kilinda (JKT Ruvu) na Charles Mkwasa (Ruvu
Shooting). Kila mshindi mepata sh. 3,875,000.
Timu
yenye nidhamu bora ni Azam iliyopata sh. 7,750,000, mshindi wa tatu
Yanga sh. 15,500,000, makamu bingwa Azam sh. 22,000,000 na bingwa Simba
sh. 50,000,000.
|
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye akimkabidhi hundi yenye thamani ya Sh. milioni 15.5 Katibu wa Yanga Selestin Mwesigwa wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar es Salaam. Anayeshudia katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa. |
|
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kushoto) akishuhudia Mwenyekiti wa Azam FC, Mohamed Said akipongezwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Vodacom, Kelvin Twisa mara baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. milioni 22 kwa kuibuka washindi wa pili katika msimu 2011/2012 wa ligi kuu ya Vodacom wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar es Salaam. |
Pia
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewazawadia sh. 1,000,000
kila mmoja kwa wachezaji watatu vijana wenye umri chini ya miaka 20
waliofanya vizuri kwenye ligi hiyo.
Wachezaji
hao ambao walikuwa kwenye vikosi vya kwanza vya timu zao ni Frank
Domayo (JKT Ruvu), Rashid Mandawa (Coastal Union) na Hassan Dilunga
(Ruvu Shooting).
No comments:
Post a Comment