Sunday, July 1, 2012

JUMA NATURE, MWASITI, ROMA WAPAGAWISHA TAMASHA SUPA 5 MTWARA

Ni mtoto toto-tundu, tukutu, kumkemea usithubutu atakutoa mkuku.... ni kighetto-ghetto.... Msanii Juma Kassim a.k.a Kiroboto akifanya mambo yake wakati wa uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani  Mtwara leo.

Mwasiti wa THT akipagawisha mashabiki wakati wa uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani  Mtwara leo.

Roma Mkatoliki "akichana" mistari wakati wa uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani  Mtwara leo.

Wacha weweeeee...... Chezea Kiduku wewe... Twende sasaaa. Mambo ya Supa 5 Mtwara hayo

: Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Amina Keita  (kushoto) akitoa zawadi ya simu kwa mmoja wa wakazi wa Mtwara, Nasra Salehe wakati wa uzinduzi wa huduma ya  Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana. Tukio hilo liliambatana na burudani kutoka kwa wasanii chipukizi wa mkoani humo na baadhi ya wasanii maarufu kutoka katika Jiji la Dar es Salaam ambako waliohudhuria walielezwa jinsi ya kujiunga na faida mbalimbali zinazopatikana katika huduma ya Supa 5.

Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akitoa zawadi ya simu kwa Jamimu Mohamed baada ya kuibuka mshindi kwa kutoa maelezo sahihi ya jinsi ya kujiunga na faida za huduma ya Supa 5 ya Airtel wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana.


No comments:

Post a Comment