Tisha mbaya...! Hapa Kanoute akionyesha vitu vyake wakati akiichezea Sevilla katika mechi mojawapo ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispani. |
Kanoute akionyesha jezi ya klabu yake mpya leo. Imeandikwaje? Mmmhh... sijui STRAIKA! |
SEVILLE, Hispania
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa kutoka Mali, Frederic Kanoute ametua nchini China leo kujiunga na
klabu ya Beijing Guoan inayoshiriki Chinese Super League, Ligi Kuu ya China.
Awali,
mshambuliaji huyo aliyekuwa akiichezea Sevilla inayoshiriki La Liga, Ligi Kuu
ya Hispania, alisema mwanozni mwa wiki kuwa anaangalia uwezekano wa kuhamia
Mashariki ya Kati, China na Marekani.
Na sasa
amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Guoan, timu inayoshika nafasi ya
tatu katika msimamo wa ligi kuu ya China, ikiachwa kwa pointi saba na vinara
Guangzhou Evergrande.
Kanoute
alisajiliwa na Sevilla mwaka 2005 baada ya kuichezea Tottenham kwa miaka miwili
na kuwa mmoja wa wachezaji nyota wa klabu hiyo, akifunga mabao 136 katika mechi
290.
Wakati akiwa
Hispania, Kanoute alitwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mwaka 2007 na pia
aliisaidia Sevilla kutwaa makombe mawili ya Uefa, taji moja la Uefa Super Cup,
makombe mawili ya Kombe la Mfalme na taji moja la Hispania la Supercopa.
Hivi
karibuni, mshambuliaji mwingine nyota wa Afrika, Didier Drogba alisajiliwa na
klabu ya China ya Shanghai Shenhua na ataripoti Julai 13 baada ya kumaliza
mkataba wake na klabu yake ya Chelsea.
No comments:
Post a Comment