Mwanamuziki mashuhuri nchini Uganda, Joseph Mayanja a.k.a Chameleon akiwa nje ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda pamoja na wapambe wake na mabango akishinikiza arejeshewe pasi yake ya kusafiria ambayo anadai inashikiliwa na Bw. Erick Shigongo baada ya kuja nchini kutumbuiza katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7 mwaka huu siku ambayo pia Diamond alitumbuiza, na waigizaji Wema Sepetu na Jacqueline Wolper walizichapa katika pambano la ndo la hisani la kuchangia ujenzi ya mabweni ya wanawake katika shule mbalimbali za sekondari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utangazaji za Uingereza (BBC), Chameleon alidai kwamba kushikiliwa kwa pasi yake hiyo kulikuwa kunamhatarishia kukosa safari yake ya kwenda nchini Uingereza kutumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa michezo ya Olimpiki unaofanyika leo jijini London. Chameleon alisema Shigongo alimpa mtu ambaye alidai kuwa ni meneja wake (Chameleon) dola 3,500 lakini "nikamfahamisha kwamba huyo si meneja wangu na sihusiki na fedha hizo. "Na kwa msaada nikamkamata huyo aliyedai kuwa ni meneja wangu akashikiliwa na polisi (wa Uganda) na nikamwambia Shigongo kwamba mtu huyo yuko polisi aje amalizane naye na mimi anirudishie pasi yangu lakini hakufanya hivyo. Alidai kwamba aliamua kuandamana baada ya kuona hapati msaada katika kudai pasi yake ambayo si mali yake binafsi bali ni mali ya serikali ya Uganda. "Niliongea na Balozi wa Tanzania nchini Uganda akaniambia nije kesho, na kesho akaniambia nije kesho... nikaona kesho-kesho zinazidi." Hata hivyo, Chameleon alifanikiwa kwenda Uingereza baada ya kupata pasi ya muda. Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Dkt. Ladislaus Komba, alielezea kushangazwa na hatua ya muimbaji huyo wa "Valu Valu' kwenda kupiga kambi nje ya ubalozi huo na hata kuondoka kwa kutuma pasi ya muda ilhali walishazungumza na kumhakikishia kwamba pasi yake ilikuwa njiani tayari imeshatumwa kutoka Tanzania. Akizungumza na kituo cha radio cha Clouds FM, Shigongo alisema: "Kila mtu anamfahamu Chameleon ni msumbufu... ili kufanya shoo alitaka dola 5,000 tukampa, mara akasema apewe dola 8,000 tukampa kwa sababu tumeshatangaza kwa watu shoo... ni msumbufu sana." |
Jose Chameleon akipiga gitaa na kuimba wakati akidai pasi yake ya kusafiria. |
Askari wakihakikisha hali inabaki kuwa salama nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Uganda wakati Jose Chameleone alipofika kwa maandamano kudai pasi yake ya kusafiria. |
Chameleone akijiandaa kulala |
Mashabiki wa Jose Chameleon wakiandamana na "boda boda" kudai kurejeshewa pasi ya kusafiria ya nyota huyo. |
No comments:
Post a Comment