Zlatan Ibrahimovic wa Sweden akifunga bonge la goli dhidi ya Ufaransa wakati wa mechi yao ya hatua ya makundi ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine Juni 19, 2012. |
Zlatan Ibrahimovic wa Sweden akishangilia goli lake dhidi ya Ufaransa wakati wa mechi yao ya hatua ya makundi ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine Juni 19, 2012. |
Zlatan Ibrahimovic akiwa katika uzi wa AC Milan |
NDEGE binafsi imeandaliwa tayari kusubiri kumchukua Zlatan Ibrahimovic kutoka Sweden hadi Paris jioni ya leo.
Mshambuliaji huyo wa AC Milan, anajiuliza kuhusu kumfuata Thiago Silva klabuni PSG, lakini wakala wake Mino Raiola anaamini kwamba dili hilo litakamilika.
Raiola alikuwa mjini Paris wikiendi kwa ajili ya mazungumzo marefu na bosi wa PSG, Leonardo kuhusu malipo binafsi ya mchezaji na vipi Ibra atashawishiwa kucheza katika 'Ligue Une', ligi kuu ya Ufaransa.
Moja ya mambo yanayofanywa kumshawishi ni kumfanya "kama mfalme", ndio maana wakamuandalia ndege binafsi.
"Nampenda Leonardo," alisema Raiola, "lakini sitatumia naye siku tatu tukinywa kahawa. Nasisitiza katika jambo moja: katika mkataba, vipengele vyote ni muhimu, na vitu muhimu vyote viwekwe kwenye vipengele. Lakini natumai tutamaliza mambo na Paris Saint Germain."
No comments:
Post a Comment