Mtaalam
wa Mitambo Haroun a.k.a Dj Run akifanya vitu vyake wakati wa Tamasha hilo.
Kampuni ya huduma za simu ya Vodacom Tanzania imefanya tamasha la Wajanja Tour mwishoni mwa wiki hii mkoani Tanga ikiwa ni kukamilisha msimu wa kwanza wa ziara hiyo ambayo ilizinduliwa Dar Es Salaam na baadae kufanyika Morogoro, Mtwara na sasa Mkoani Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema kuwa tamasha hilo lilifanyika katika uwanja wa mkwakwani ikiwa ni katika kukamilisha msimu wa kwanza wa mfululizo wa matamasha yaliyofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
“Tamasha hili la Mkoa wa Tanga katika uwanja wa Mkwakwani lilifanyika katika kukamilisha msimu huu wa kwanza. Tunajipanga kwa ajili ya msimu wa pili wa kutoa burudani kwa watanzania. Tunawahakikishia wateja wetu kuwa tamasha hili halitaishia hapa, tunaangalia namna ya kwenda katika mikoa mingine kwani watu wengi wamevutiwa na burudani wanayoipata hivyo tunaangalia uwezekano wa kwenda mikoa mingine ya Tanzania bara na visiwani,” alisema Nkurlu.
“Lengo la Tamasha la Wajanja Tour sio tu kutoa burudani, pia ni njia pekee ya kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kupata nafasi ya kuendelea vipaji vyao zaidi kama ambavyo mmeshuhudia katika matamasha mbalimbali vijana wengi wamepata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa kuimba,” alisema.
Tamasha la Wajanja wa Vodacom limekuwa na lengo la kuwahamasisha vijana kujiunga na kupata huduma kutoka mtandao wa Vodacom Tanzania ambapo kampuni hiyo imeanzisha huduma mbalimbali ambazo zinaweza kurahisisha matumizi ya simu kwa kuongea kwa robo shilingi, kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano kwenda mtandao wowote hapa nchini na kuperuzi facebook na twitter bure. Pia wateja wa Vodacom wananufaika sana na huduma ya intanet hasa vijana ikiwemo ofa ya wajanja intanet inayompa mteja huduma ya intaneti kwa shilingi 250 kwa siku, pamoja na ofa ya simu za Nokia Asha kwa shilingi elfu sabini na tano tu.
|
No comments:
Post a Comment