Jaji Mkuu wa Epiq Bongo Star Search, Ritha Paulsen (kulia) akiwaliwaza washiriki wa shindano hilo mkoani Arusha. |
Jaji wa Epiq Bongo Star Search, Master Jay (kulia) akimliwaza kijana aliyeshindwa katika mchujo wa shindano hilo mkoani Arusha. Jumamosi hii mambo ni Mwanza. |
Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kumaliza ziara ya kusaka vipaji mikoa ya Arusha, Lindi, Zanzibar na Dodoma, majaji wa Epiq Bongo Star Search sasa wamejiandaa kupata vipaji kutoka mkoa wa Mwanza hapo Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani hapa.
Mkoa wa Mwanza ambao unasifika kwa kutoa wasanii wakali kama Marehemu James Dandu na Farid Kubanda maarufu kama Fid Q, unatarajiwa kuleta ushindani mkali ukizingatia mshindi wa mwaka jana, Pascal Cassian alitoka mkoani hapa.
Akizungumzia mkoa wa Mwanza Jaji Mkuu wa Epiq Bongo Star Search 2012 Ritha Paulsen alisema kuwa wamejipanga kupata vipaji luluki na vikali kutoka Mwanza.
“Mimi kama mdau wa sanaa najua kuwa Mwanza kumekuwa na harakati za muziki muda mrefu, watu kama James Dandu, wametokea Mwanza, hivyo tumejipanga na majaji wenzangu kuhakikisha tunapata vijana watakaoweza kuiwakilisha Mwanza vizuri,”alisema Ritha.
Aliongeza kuwa kwa Epiq BSS, Mwanza ni mojawapo ya mikoa ambayo vijana wengi hujitokeza kuwania nafasi ya kuingia kwenye shindano hilo maarufu nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Deepak Gupta, alisema Wanamwanza watarajie zaidi ya kusaka vipaji kwani kutakuwa na shughuli nyingi zitakazoendelea mkoani hapa.
"Shindano hili ndio maana tunaliita Epiq, kila kitu ni zaidi, tutakuwa na shughuli za utoaji damu pamoja na shughuli nyingine za kijamii, lakini pia kwa upande wa burudani tutakuwa nazo za kutosha," alisisitiza Gupta.
-----------
No comments:
Post a Comment