MKUTANO NA WAHARIRI WA MICHEZO
Clement Sanga akizungumza na Waandishi wa Habari |
NDUGU
zangu wanahabari, nimewaiteni leo kuzungumza nanyi kama mnavyofahamu nawania
nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga.
Nimejitosa
kuwania nafasi hii nikiamini nina uwezo na sababu ya kuiongoza Yanga, ili
niweze kutoa mchango wangu kwa klabu ninayoipenda tangu utotoni.
Ili
ndoto za yale ninayofikiri ni muhimu katika vipaumbele vyangu, kwa kushirikiana
na viongozi wenzangu sanjari na wanachama, kwanza kabisa kutengeneza mfumo
ambao mipango yake inatekelezeka.
Mfumo
huo wa awamu tatu tofauti, tukianzia mipango ya muda mfupi, muda wa kati na
mipango ya muda mrefu, ambao hata kama muda wetu wa kukaa madarakani
utamalizika, itawawia rahisi viongozi wajao kuongoza kwa kufuata mfumo zaidi
ambao utarahisiha utekelezaji wa majukumu yao.
Kama
nikipata ridhaa ya kuiongoza Yanga kuna mambo ambayo nitayapa kipaumbele
ikiwemo suala la marekebisho ya Katiba.
Kwa
kushirikiana na viongozi wenzangu, lakini kwa kuwashirikisha zaidi wanachama tutaipitia
upya Katiba na kuifanyia marekebisho, ili tuwe na Katiba imara, yenye nguvu
itakayoletea tija.
Kwa
sasa Yanga haina dira wala mwelekeo. Tunahitaji kuwa na dira na mwelekeo, bila hivyo
hatutafika popote, hivyo nikiingia madarakani kwa kushirikiana na viongozi
wenzangu mtazamo wangu utakuwa katika kujenga mfumo wa kudumu katika masuala
yafuatayo.
(1)
Umoja:
Kusimamia suala la umoja na mshikamano ndani ya klabu na kuondoa makundi na
kuhakikisha Yanga inakuwa moja kwani haiwezekani mwana- Yanga adui yake, awe
mwana Yanga, hivyo umefika wakati mambo hayo yaondolewe.
Ili kuimarisha uhusiano na kujenga umoja ndani ya
Yanga, tutahakikisha vikundi vyote vilivyomo ndani ya klabu vinatambuliwa
kikatiba ili viweze kuendelea kuisaidia klabu kwa utaratibu ulio rasmi.
Hii nikimaanisha viongozi wa matawi Tanzania
nzima, Wazee, vijana na hata vikundi vya ushangiliaji vinavyoleta hamasa katika
michezo yetu mbalimbali.
(2)
Soka
la vijana: Nitahakikisha natilia mkazo kuendeleza soka la vijana na kuibua
vipaji vipya kama ilivyokuwa miaka ya zamani.
Mpira
si kama paa la nyumba kwamba siku zote linakuwa juu tu, soka inaanza chini
hivyo ni vyema watu wakatambua hilo, ili mchezo huu upige hatua kama zilivyo
nchi zilizoendelea duniani, ni lazima utengenezwe msingi kwanza kwa kuchagua
vijana wadogo, ambao baadaye watakuwa hazina kwa Yanga.
(3)
SACCOS-
Kuwafanya wana Yanga wajivunie zaidi klabu yao, tutapanua wigo wa taasisi yetu,
kwa kuanzisha Mfuko wa Akiba na Mikopo kwa wanachama (SACCOS), ambao utakuwa
ukitoa mikopo kwa wanachama wake, kupitia matawi jambo ambalo litaondoa
utegemezi katika klabu na hata miongoni mwa wanachama.
(4)
KUJITEGEMEA:
Tutabadili mfumo wa uendeshaji klabu uendane na hali ilivyo ya soka la sasa,
ambapo klabu inatakiwa kujiendesha kibiashara, kwani Yanga ni taasisi kubwa
yenye fedha nyingi, ambazo zikitumika ipasavyo, zitaisaidia timu kiuchumi na
kujiendesha kisasa na jambo hilo litawezekana iwapo tutakuwa na Katiba bora
ambayo itawezesha jambo hilo kutekelezeka kiurahisi.
Ni aibu klabu kubwa kama Yanga kuwa maskini,
wakati ina raslimali za kutosha ambazo haziinufaishi, hivyo kubadili mfumo wa
uendeshaji kutaifanya iweze kujiendesha kwa kujitegemea.
Nia sio kurudi nyuma bali kwenda mbele na
kuondoa umaskini uliokithiri katika klabu yetu na kuifanya ijiendeshe kisasa na
kuwa klabu ya kulipwa ambayo inaweza kukabiliana na klabu nyingi kubwa za
Afrika.
Kwa
kushirikiana na viongozi wenzangu nitaweka mawazo ya kuifanya Yanga iweze
kujiendesha kibiashara na ikiwezekana kubadili katiba kwa kutilia mkazo suala
la kampuni ili tuweze kuuza hisa za klabu, jambo ambalo litasaidia kuongeza
mapato pamoja na kuwajibika kwa wanachama ambao sasa watakuwa sehemu ya klabu
kwa karibu zaidi.
(5)
UENDESHAJI
WA KLABU: Pia katika kuboresha mfumo huu wa uendeshaji, tutaunda idara kadhaa
kwa ajili ya kurahisisha suala hilo, ambapo kutakuwa na Idara za Uhasibu,
Masoko, Sheria pamoja na ile ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano.
Pia
shughuli zote zinazohusu klabu zitafanyika makao makuu ya klabu yetu Jangwani,
hivyo mawasiliano yoyote ya kikazi baina ya wachezaji, viongozi, wanachama na
wadau wa Yanga yatafanyika klabuni lengo ni kuongeza heshima na uadilifu kwa Yanga.
Ili
kulipa nguvu suala hilo tutalifanyia ukarabati jengo la makao makuu ya klabu liwe
na hadhi ya Yanga na kwa ujumla uongozi wangu kwa kushirikiana na wenzangu
utakuwa ule unaozingatia zaidi Katiba.
(6)
MATAWI:
Nitahahakikisha uongozi wangu unaimarisha matawi ya klabu na kufanya wanachama
kufahamu na kuchangia shughuli za klabu na kwa kuanzia itakuwa busara kila
wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam kuwa na ofisi na vitendea kazi muhimu na mpango
huo utaendelea nchi nzima.
Lakini
pia lazima niwe muwazi tangu sasa, kuwa si kila jambo litahusisha wanachama
wote, mfano mipango ya timu kwa maana ya
usajili, ushiriki wa ligi na michuano ya Kimataifa, hilo likishikwa na watu
wengi nafasi yake ya mafanikio huwa ndogo, tutazipa nguvu kamati za ufundi na
mashindano kufanya kazi kwa wepesi na ushirikiano mkubwa.
KAULI
YANGU KWA WANA-YANGA:
Naomba
wanichague mimi wajenge imani kwangu kwani nitahakikisha kwa kushirikiana na
wenzangu tunajenga timu imara ya ushindani, itakayokuwa tishio katika michuano
ya ndani na ya kimataifa. Wamchague Sanga kwa Yanga inayoeleweka.
SANGA
KWA YANGA INAYOELEWEKA.
Sanga kushoto akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Namanga, Dar es Salaam |
Clement Sanga. Picha zote: www.http://bongostaz.blogspot.com/ |
No comments:
Post a Comment