Fabio Capello |
MOSCOW,
Urusi
KOCHA wa
zamani wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello ameapa kubadili soka la Urusi
na kuifanya timu ya taifa hilo kuwa moja ya timu kali duniani ikiwa ni muda
mfupi tu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu hiyo leo.
Muitalia
Capello anachukua nafasi ya Mholanzi Dick Advocaat, ambaye kibarua chake
kiliota mbawa kufuatia matokeo mabaya waliyopata Urusi katika fainali za Euro
2012, ambazo waliishia katika hatua ya makundi.
Kocha huyo
mwenye miaka 66, alionekana akiwa amevalia suti ya kijivu na tai ya bluu nyeusi.
Hakuchelewa kuahidi mbele ya waandishi wa habari jijini Moscow kwamba atafanya
kazi yake kwa ukamilifu.
"Najivunia
kuwa kocha wa timu ya taifa ya Urusi. Kuna vipaji vingi Urusi. Nitaishi na
kufanya kazi jijini Moscow," alisema.
Taarifa za
vyombo vya habari vya Urusi zimedai kuwa atakuwa akilipwa mshahara wa euro
milioni 10 kwa mwaka (Sh. bilioni 20)
No comments:
Post a Comment