Mkurugenzi wa TANESCO, Eng. Mhando |
Habari zilizofika punde na kuripotiwa pia katika Televisheni
ya Taifa (TBC1) zinasema kuwa Meli ya Sahara II inaendelea kuteketea kwa moto baada
ya kufika Mafia ikitokea jijini Dar na mizigo ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Kamanda wa wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu amekaririwa
akisema kuwa jitihada za kuzima moto huo bado zinaendelea.
Imeelezwa zaidi kuwa Wilaya ya Mafia haina gari la zimamoto,
hivyo wananchi wanendelea kufanya jitihada za kuzima moto huo kwa kutumia mikono
na maji.
No comments:
Post a Comment