Boti ya Mv Sepideh ikiwa katika bandari ya Zanzibar tayari kwa kuanza safari. |
Boti maarufu
ya kusafirisha abiria ya Mv Sepideh nayo imefutiwa rasmi hati ya kufanya kazi visiwani Zanzibar leo na kuungana na boti nyingine za Mv Kalama na Mv Skagit zinazomilikiwa na kampuni ya Seagull Sea Transport Company Limited, imefahamika.
Hatua hiyo
imetangazwa leo na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar baada ya kubaini kwamba boti
hizo hazikidhi vigezo vya kujihusisha na shughuli za kusafirisha abiria.
Boti ya Mv Sepideh ni miongoni vya vyombo maarufu kwa usafirishaji wa abiria kati ya jiji la Dar es Salaam na Zanzibar.
Hatua ya kusimamishwa kwa boti hiyo na nyingine imekuja ikiwa ni siku chache tu baada
ya tukio la kuzama kwa Mv. Skagit inayomilikiwa na Kampuni ya Seagull Sea
Transport Company Limited katika eneo la Chumbe ikitokea jijini Dar es Salaam na
kusababisha upotevu wa mali na vifo vya watu 123 hadi kufikia leo.
No comments:
Post a Comment