Olivier Giroud |
MSAKA vipaji wa Arsenal, Gilles Grimandi amekiri kwamba klabu hiyo imemsajili Olivier Giroud ili kuziba pengo la Robin van Persie kama ataondoka.
Nahodha huyo wa Arsenal amesisitiza kwamba hatasaini mkataba mpya, huku mkataba wake wa sasa ukiwa unamalizika mwisho wa msimu ujao, na amehusishwa na mipango ya uhamisho wa pesa nyingi wa kwenda Manchester City.
Arsenal imemsajili straika wa timu ya taifa ya Ufaransa, Giroud na kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Lukas Podolski, jambo ambalo litaimarisha safu yao ya ushambuliaji msimu unaokuja.
Grimandi amesema: "Tunataka (van Persie) abaki, lakini amebakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake hivyo mambo yanakuwa magumu mno.
"Hali iko poa klabuni Arsenal, amekuwa nasi kwa miaka nane na amekuwa na muunganiko muhimu na klabu.
Giroud akiwa katika jezi itakayotumiwa na Arsenal msimu ujao |
"Je, Olivier Giroud alisajiliwa ili kuziba pengo lake akiondoka? Ndio, tulifanya hivyo ili kuepuka kujikuta "kitanzini".
"Lakini tunafanya kila tunaloweza ili abaki na tunataka abaki nasi.
"Hata hivyo, kama kuna ofa ya kipekee na anataka kuondoka, kumbakisha itakuwa ngumu.
"Sikuwahi kufikirikia, kwa mfano, kwamba Thiago Silva anahamishika Milan. Lakini kuna mambo mbalimbali ambayo hayadhibitiki."
No comments:
Post a Comment