ANDREA
Pirlo, ambaye ameng'aa soka la dunia kutokana na utawala wake katika Euro 2012,
haamini kama anastahi kutwaa tuzo ya FIFA Ballon d'Or mwaka huu kwa sababu
hajafunga magoli ya kutosha.
Kiungo
huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye timu yake ya Italia leo usiku itaikabili
Ujerumani katika nusu fainali ya Euro 2012, hajawahi kuwa mfungaji sana kutokea
katika nafasi yake ya nyuma ya kiungo lakini ameacha gumzo katika michuano
hicho kutokana na penalti yake ya kudokoa wakati wa kupigiana "matuta"
katika mechi ya robo fainali dhidi ya England.
Alipoulizwa
kama anadhani anastahili kutajwa mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa
Mwaka baada ya pia kuiongoza Juventus kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia
(Serie A) mwezi Mei, mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2006 alikataa.
"Hapana,
kuna (Lionel) Messi na (Cristiano) Ronaldo. Ni jambo lisilowezekana kuwa mbele
yao," aliuambia mkutano na waandishi wa habari uliowahusisha wanahabari
kutoka nchi mbali kama Marekani na China.
"Wao
wamefunga magoli mengi sana. Sidhani kama naweza hata kujadiliwa."
------------
No comments:
Post a Comment