Bila watu watatu hazuiliki...Hapa Iniesta akijaribu kuwachambua kama karanga wachezaji wa Ufaransa katika Euro 2012. |
Kweli Iniesta noma! Hapa machachari yake yanamfanya alindwe vikali ni wachezaji walioshiba wa Italia katika mechi yao ya hatua ya makundi ya fainali za Euro 2012. |
Kiungo mchezeshaji
wa Hispania, David Silva amesema atampa nafasi ya kwanza mchezaji
mwenzake wa kimataifa wa Hispania, Andres Iniesta kuwa mchezaji bora wa Dunia kabla ya nyota wawili
wanaochukuliwa kuwa ndio bora zaidi katika miaka ya hivi karibuni, Lionel
Messi na Cristiano Ronaldo.
Hispania wanacheza
dhidi ya Uren leo usiku katika mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012, huku Silva
na Iniesta wakitarajiwa kuvaana uso kwa uso na Ronaldo, ambaye ameng’ara katika
michuano hiyo tangu ‘alipochemsha’ katika mechi mbili za ufunguzi za hatua ya
makundi dhidi ya Ujerumani na Denmark.
Iniesta pia
amekuwa akionyesha kiwango cha juu tangu kuanza kwa michuano hiyo na hadi sasa
ana wastani wa kutoa pasi zinazowafikia wenzake kwa asilimia 91, lakini ni mchango wake wa
jumla katika kikosi cha Hispania ndio unaomfanya Silva ammiminie sifa, akigusia
ni kwa namna gani amekuwa mhimili wa kikosi chao kinachofundishwa na kocha Vicente
del Bosque.
“Waandishi wa
habari kila mara wamekuwa wakiniuliza kuhusu Messi na Ronaldo na nani kati yao ni bora
zaidi, lakini kitu kimoja kwangu kiko wazi kabisa," Silva aliwaambia
waandishi wa habari.
“Kwangu mimi,
No.1 kwa ubora ni Andres Iniesta kwa sababu ni mchezaji mwenzangu katika kikosi
cha Hispania na ninaweza kuona kwamba ana uwezo wa kufanya vitu adimu uwanjani.
Andres ni mchawi awapo na mpira na pia ni mtu poa, mchezaji nyota kikosini.
“Siwajui kiundani
Ronaldo wala Messi, lakini Andres ni mchezaji nyota na pia ni mtu poa. Muhimu
sana kikosini.
“Ureno wana
timu nzuri na wanacheza soka safi. Wameonyesha vilevile kwamba wao si Ronaldo
tu. Sisi hatujapania mechi hii kwa sababu tu ya kucheza dhidi ya Ronaldo... tuko tayari kucheza dhidi ya timu ya Ureno.“
No comments:
Post a Comment