LUGHA chafu iliyotolewa na Samir Nasri dhidi ya mwandishi wa habari kufuatia kipigo cha Ufaransa cha 2-0 kutoka kwa Hispania katika mechi yao ya robo fainali ya Euro 2012 Jumamosi ilikuwa ni "mbaya, mbaya mno" kwa sifa yake, kocha Laurent Blanc amesema.
"Ni jambo la kujutia lakini ni matatizo binafsi
baina ya Samir na vyombo vya habari. Ni mbaya, mbaya sana kwa sifa yake lakini
jambo hili linapofanywa wakati yuko katika timu ya Ufaransa ni mbaya kwa sifa
ya timu," Blanc alikiambia kituo cha televisheni cha TF1 cha Ufaransa
jana.
"Kwa mujibu wa ninachofahamu, alikosa heshima kwa
mwandishi ambaye pia kwa wakati fulani alimkosea heshima Nasri."
Kiungo Nasri tayari alihusika katika majibizano na vyombo
vya habari katika michuano hiyo wakati alipoonyesha ishara ya "funga
domo" baada ya kufunga goli la kusawazisha la Ufaransa katika sare ya 1-1
dhidi ya England katika mechi yao ya ufunguzi.
"Nilimweleza nilichofikiria kuhusu jambo hili (baada
ya tukio la kwanza) lakini naona ujumbe haukumuingia," aliongeza Blanc.
No comments:
Post a Comment