Majaji wa Epiq Bongo Star Search 2012, kutoka kulia Salama
Jabiri, Madam Ritha na Master J wakimsikiliza mmoja wa washiriki kwa umakini.
|
Na Mwandishi Wetu
UWANJA wa burudani uliopo katika eneo la Ngome Kongwe leo ulifurika maelfu ya vijana waliojitokeza kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuchaguliwa kuingia katika fainali za shindano la Epiq Bongo Star Search 2012.
Huku kukiwa na idadi kubwa ya washiriki wasichana pia kulikuwa na washiriki ambao waliwasili wakiwa na vifaa mbalimbali vya kupigia muziki kama vile gitaa, vinanda na vinginevyo ikiwa ni mikakati yao ya kujihakikishia kuchaguliwa.
Akizungumzia usaili wa Zanzibar, Jaji Mkuu wa EBSS 2012, Ritha Paulsen alisema kuwa ameguswa na mwamko wa washiriki kutoka Zanzibar.
Mkuu wa mawasiliano wa kampuni ya huduma za simu ya Zantel
Awaichi Mawala (kushoto) akijumuika kuimba na washiriki waliojitokeza katika
usaili huo.
|
"Zanzibar ina vijana wengi wenye vipaji na ambao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia malengo yao katika muziki," aliongeza Ritha.
Alisema kuwa kupitia shindano la EBSS ambalo linadhaminiwa na kampuni ya huduma za simu ya Zantel anatarajia kupata vipaji vingi katika mikoa yote ambayo usaili unaendelea.
Naye Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel kwa Zanzibar, Mohamed Mussa mbali na kufurahishwa na idadi kubwa ya washiriki waliojitokeza aliwataka vijana wa kisiwani hapa kutambua kuwa muziki unaweza kuwapatia ajira kubwa.
"Muziki ni ajira, na ndio maana sisi Zantel tumeamua kuwekeza kwenye mashindano haya ili kuwapa fursa vijana wengi zaidi," alisisitiza Mussa.
No comments:
Post a Comment