Friday, June 29, 2012

NANI AMSHUKIA RONALDO: ALING'ANG'ANIA PENALTI YA MWISHO

Cristiano Ronaldo wa Ureno (kulia) akionekana kufadhaika baada ya timu yao kutolewa kwa "matuta" dhidi ya Hispania wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Donbass Arena Juni 27, 2012 mjini Donetsk, Ukraine.
 
NANI amemshukia nyota mwezake wa zamani wa Manchester United,  Cristiano Ronaldo, kuhusu "kashfa" ya upigaji wa penalti katika mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 waliyotolewa kwa "matuta" dhidi ya Hispania.

Ronaldo ameshambuliwa vikali kwa kutojitokeza mapema kupiga penalti katika mechi hiyo waliyolala kwa penalti 4-2 bila ya nyota huyo wa Real Madrid kupiga yake baada ya  Bruno Alves, ambaye ni beki, kugongesha penalti yake kwenye "besela".

"Cristiano Ronaldo aling'ang'ania kupiga penalti ya mwisho," winga huyo alisema. "Mimi nilimwambia kocha nitakubali amri ya mtiririko wowote.

"Haikuonekana kuwa tatizo kwangu, kwa sababu upigaji wa penalti unategemea bahati tu na hatukustahili kufungwa namna ile."

Ronaldo ameshutumiwa kutaka kupiga penalti ya "ujiko" ili aje kubebwa kama shujaa baada ya mechi, jambo ambalo halikumfikia kwani Cesc Fabregas alifunga penalti ya 4-2, na hivyo kutokuwepo umuhimu wa Ronaldo kumalizia yake ya tano.

No comments:

Post a Comment