MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City iko mbioni kuandaa mkataba mnono ili kumnasa mshambuliaji Robin van Persie wa klabu ya Arsenal.
Gazeti la Daily Star limesema kwamba Man City wako tayari kumlipa Van Persie mshahara wa paundi za England 225,000 (Sh. Milioni 540) kwa wiki ili kumng’oa nahodha na mshambuliaji huyo nyota wa Arsenal.
Imeelezwa zaidi kwamba mchezaji huyo ndiye No. 1 miongoni mwa washambuliaji wanaotakiwa na kocha Roberto Mancini na ndio maana uongozi wa Man City uko tayari kumpa dau ambalo kamwe hatakuwa na ubavu wa kulikataa.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amepania kumbakisha Van Persie, lakini itakuwa vigumu kwani ni wazi kwamba Van Persie hawezi kudengua mshahara huo wa Sh. Milioni 540 kwa wiki atakaoupata pindi akitua Man City.
No comments:
Post a Comment