Guardiola akionyesha tuzo aliyotwaa ya Kocha Bora wa Mwaka wa Dunia 2011 |
KUALA LUMPUR, Malaysia
Pep Guardiola amekiri kwamba tayari ameanza kuhisi kuwa ‘amemisi’
soka ikiwa ni wiki chache tu baada ya kujiondoa katika nafasi ya kuwa kocha wa Barcelona.
Kocha huyo aliyeandika rekodi ya kuwa mwenye mafanikio kuliko wote waliowahi kuifundisha Barca, aliamua kutosaini mkataba mwingine wa
kumbakisha Camp Nou baada ya kudumu kwa miaka minne, akidai kwamba uchovu ndio
sababu kubwa ya kuondoka kwake.
Hata ahivyo, kocha huyo mwenye miaka 41 amesema kwamba tayari
ameanza kutamani kurejea katika masuala ya soka, kabla hajatania kwa kusema kuwa
ameshachoka kuendelea kucheza gofu.
"Ninatamani soka? Kiukweli nimeanza kulimisi soka. Nimeshachoka
kucheza gofu na baba yangu," Pep aliwaambia waandishi wa habari wakati wa
ziara yake mjini Kuala Lumpur, Malaysia.
Guardiola aliiongoza Barca kutwaa mataji 14 wakati wa kipindi
chake cha miaka minne. Nafasi yake imerithiwa na aliyekuwa msaidizi wake, Tito
Vilanova na kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda Chelsea.
No comments:
Post a Comment