Thursday, June 28, 2012
FABREGAS ANA KIZIZI TIMU YA TAIFA HISPANIA
MCHEZAJI aliyeingia kutokea benchi Cesc Fabregas ana "kizizi" cha kupika mafanikio pale yanapohitajika kwa timu ya taifa ya Hispania.
Penalti yake ya ushindi dhidi ya Ureno wakati wa kupigiana "matuta" katika mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 jana usiku, iliongeza mkusanyiko wa matukio yake ya kuipa mafanikio Hispania baada ya kupiga pasi ya mwisho iliyozaa bao lililoipa nchi yake ubingwa wao kwanza wa katika historia ya Kombe la Dunia 2010.
Italia pia wataikumbuka penalti yake ya ushindi baada ya kuingia akitokea benchi katika mechi yao ya robo fainali katika michuano iliyopita ya Euro.
"Nilikuwa na hisia za masihara kuhusu upigaji wa penalti na nilikuwa nazifikiria jioni hii. Kwamba maisha yamenipa fursa nyingine kama hii ni jambo kubwa," Fabregas alisema baada ya ushindi wa Hispania wa 4-2.
"Niliposogea kupiga penalti ile niliuambia mpira kwamba tunataka kuweka historia na haupaswi kuniangusha. Awali waliniambia nikapige penalti ya pili lakini nikasema hapana nipeni ya tano kwa sababu nina bahati."
Kujiamini kwa Fabregas kukathibitisha kulikuwa sahihi zaidi ya imani ya Ureno kumuacha mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo aje kupiga penalti ya mwisho.
Mchezaji huyo ghali zaidi duniani alibaki amesimama kama mtu aliyekosa msaada wakati akimshuhudia kiungo wa Barcelona, Fabregas, akizima ndoto za Ureno katika michuano hiyo.
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment