MARIO Balotelli hana mpango wa kurejea Italia baada ya fainali za Euro 2012 — hata kama atarudi akiwa shujaa wa taifa.
Mshambuliaji huyo amesema atabaki Manchester City ambako, amesema, mashabiki wanampenda.
Jambo hilo lipo licha ya mchango wa Balotelli katika kuitoa timu ya taifa ya England katika robo fainali ya Euro wikiendi iliyopita.
Man City waliipa Inter Milan paundi milioni 22 kwa ajili ya kumsajili Balotelli mwaka 2010 lakini sasa klabu za Italia linachuana kutaka kumrejesha nyumbani.
Alipoulizwa kama atahama, Balotelli alisema: "Kurudi nyumbani sasa? Nitarejea Manchester.
"Mashabiki wa Man City daima wananihitaji, licha ya kwamba wao ni Waingereza — na nimesaidia kuitoa timu yao ya taifa."
Baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani, Balotelli anajiandaa kucheza mechi kubwa zaidi maishani mwake dhidi ya Hispania katika fainali ya Euro 2012 kesho.
No comments:
Post a Comment