Friday, June 29, 2012

BALOTELLI 'HAFAI', AFUNGA MAGOLI YA HATARI, AIPELEKA ITALIA FAINALI KUIKABILI HISPANIA

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli (kulia) akifunga goli lake la pili dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli akishangilia goli lake la pili dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli (katikati) akishangilia goli lake la pili dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli akifunga goli lake la pili dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli akishangilia goli lake la pili dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli akifunga goli lake la kwanza dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

Muunganiko wa picha zinazomuonyesha Mats Hummels (kushoto) wa Ujerumani akijaribu kufunga dhidi ya kipa wa Italia, Gianluigi Buffon wakati wa mechi yao ya nusi fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

WARSAW, Poland
MSHAMBULIAJI wa Italia, Mario Balotelli alifunga magoli mawili "makali" ya kipindi cha kwanza na kuipa timu yake ushindi wa 2-1 dhidi ya timu iliyokuwa ikipewa nafasi ya Ujerumani usiku wa kuamkia leo na kuwapeleka fainali ya Euro 2012 ambako watakutana na Hispania.

Balotelli alifunga magoli hayo mawili ndani ya dakika 16 na kuwanyamazisha waliokuwa wakimshutumu kwa kucheza soka la kiwango cha juu kilichohitimisha mwendo mzuri wa Ujerumani wa kushinda mechi 15 mfululizo katika mechi za kimashindano na kuleta fainali ambayo haikutarajiwa dhidi ya mabingwa wa Ulaya na dunia ambao walitoka nao sare ya 1-1 katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Kiungo wa Ujerumani, Mesut Ozil alifunga penalti katika dakika za majeruhi baada ya Federico Balzaretti "kuunawa" mpira ndani ya boksi lakini Italia walilinda ushindi wao. Wajerumani sasa hawajawahi kushinda mechi hata moja kati ya nane za kimashindano walizokutana na Waitalia katika kipindi cha nusu karne.

Ujerumani almanusura watanguliwe katika dakika za awali wakati kichwa cha nyuma cha Sami Khedira kilipotua kwa Antonio Cassano ambaye alimpasia Balotelli lakini mpira ulidakwa na kipa Manuel Neuer.

Cassano, ambaye maisha yake ya soka yalikuwa shakani baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mwaka jana, alirejea katika kiwango chake bora cha "upishi", akiichana safu ya ulinzi ya Ujerumani kwa pasi "tamu" na kuzua matatizo mfululizo kwa beki wa kulia wa Ujerumani, Jerome Boateng.

Andrea Pirlo aliwaokoa Waitalia katika dakika ya tano wakati Mats Hummels alipoiwahi kona ya Bastian Schweinsteiger lakini shuti lake liliokolewa juu ya mstari na kiungo huyo aliyeng'aa katika michuano hii.

Waitalia, kama kocha wao Cesare Prandelli alivyoahidi, hawakuliacha soka lao la kushambulia ili "wapaki basi" na badala yake waliendelea kupeleka mashambulizi mpaka dakika ya mwisho.

No comments:

Post a Comment