Friday, June 29, 2012

ALEX WA MACHEJO AWAPANDISHA MASTAA KWENYE NDEGE AKIREKODI VIDEO YAKE MPYA

Alex wa Machejo (kushoto) akishambulia pamoja na mchekeshaji wa kipindi cha 'Mizengwe' cha ITV, Mkwere, wakati wa kurekodi video ya wimbo wake wa 'Ngekewa'.

Alex wa Machejo (kushoto) akiwa ndani ya ndege ya Precision Air wakati wa kurekodi video ya wimbo wake wa 'Ngekewa'

Alex wa Machejo akiwa katika chumba cha rubani wa ndege ya Precision Air wakati wa kurekodi video ya wimbo wake wa 'Ngekewa'.

Alex wa Machejo (katikati) akiwa pamoja na wachekeshaji wa kipindi cha 'Mizengwe' cha ITV wakati akirekodi video ya wimbo wake wa 'Ngekewa'.

Alex wa Machejo (wa pili kushoto) akiwa pamoja na nyota wa Bongo Muvies, BIG, wakati akirekodi video ya wimbo wake wa 'Ngekewa'.
MSANII wa vichekesho katika kituo cha televisheni cha ITV, Alex wa Machejo, amerudia kurekodi video ya wimbo wake wa 'Ngekewa', mara hii akiurekodi ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air akiwa na mastaa kibao wa filamu na komedi.

Katika video hiyo amerekodiwa akiwa amekaa kwenye chumba cha rubani wa ndege hiyo na kisha katika eneo la abiria akijiachia na nyota hao wa maigizo akiwemo BIG, Mkwere na wachekeshaji wa kipindi cha Mizengwe cha ITV.


Wimbo huo umerekodiwa katika studio ya Kiri Records chini ya mtayarishaji C9 na wakati wowote video ya wimbo huo itaanza kurushwa hewani katika vituyo vya televisheni.


"Itakuwa kama ngekewa...," kinasema kiitikio cha wimbo huo. "Mimi siwezi kwenda China kucheza mpira na Ronaldo wa Yanga/ Siwezi kuwa kama Mrisho Ngassa wa Barcelona/ Tanzania kuipiga Vietnam/ Bush kutibiwa Dar es Salaam/ mtu kupigwa bomu anakuwa na akili timamu/ Rambo kucheza Bongo Muvie/ Feri kutokuuzwa uduvi/ itampa taabu Mheshimiwa Lukuvi/ Mourinho kufundisha Stars/ Eto'o kuchezea Manyema. TFF si watasema/ Afande Kaloli kumpiga John Cena naona kama ngekewa... Bi. Kidude kuimba hip hop," inasema sehemu ya mashairi.


"Wazo la wimbo huu ni tofauti kabisa, ni komedi, ni kitu ambacho hakijawahi kutokea, nimeimba vitu ambavyo havipo lakini kwa mtazamo wangu vinawezekana kutokea," anasema Alex wa Machejo, ambaye pia amekuwa akifahamika kama 'Bingwa wa Rivasi'.


Katika kituo cha ITV, Alex wa Machejo anaigiza kupitia kikundi cha Jakaya Theatre ambacho kimesharusha maigizo kama "Taharuki", "Kivuli", "Mwiba", "Kovu la Siri", "Riziki", "Kivuko", "Mapiku". "Utelezi" na kadhalika.




No comments:

Post a Comment