Sunday, January 13, 2013

BILA YA RONALDO, REAL MADRID TAABANI

'Jembe'.... Ronaldo hakucheza kwa sababu ya kadi tano za njano

Njano ya pili hii nenda nje... Kaka (wa pili kushoto) akionyeshwa kadi ya njano ya pili ndani ya dakika 18 tangu aingie uwanjani katika kipindi cha pili

Benzema akiwania mpira wa kichwa

Ozil (10) akipigwa pini

Sio goli umeotea... Callejon akifunga goli ambalo lilikataliwa kwa kuotea

Callejon akzidiwa kuruka

Dah ukuta huu haupitiki.... Karim Benzema (kushoto) akiwa haamini anachokiona
 
REAL Madrid jana usiku ilicheza kwa kiwango kibovu wakati ilipotoka sare ya 0-0 dhidi ya timu inayoburuta mkia ya Osasuna katika mechi ambayo walimkosa nyota wao Cristiano Ronaldo aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi za njano tano.

Kaka aliingia uwanjani akitokea benchi katika kipindi cha pili na alitolewa kwa kadi mbili za njano ndani ya dakika 18 katika mechi ambayo Osasuna walistahili kushinda. Real walipiga shuti la kwanza langoni kwa Osasuna katika dakika ya 93.

Kukosekana kwa Ronaldo, Pepe aliyefanyiwa upasuaji na Sergio Ramos aliyefungiwa mechi tano kwa kumtukana refa katika mechi ya Kombe la Mfalme Jumatano, hakuwezi kuwa ni kisingizio cha timu ya Jose Mourinho, ambayo iliwatumia washambuliaji Gonzalo Higuain na kisha Karim Benzema, kushindwa kufunga goli hata moja. Callejon alidhani ameifungia Real goli katika dakika za lalasalama, lakini alikuwa tayari amepigiwa firimbi ya kuotea.

Real Madrid imekuwa ikihaha kupata magoli kila alipokosekana Ronaldo, takwimu zinathibitisha. Akiwamo uwanjani CR7, Madrid haijashinda asilimia 25 ya mechi zao. Akikosekana, asilimia hiyo huongezeka hadi 35%.

Kwa ufupi: bila ya Cristiano, Madrid hupeteza mechi moja katika kila tatu.

Cristiano amecheza mechi 172 tangu awasili Madrid, ambapo wameshinda mechi 129, sare 24 na vipigo 19. Katika mechi 23 ambazo Mreno huyo amekosekana uwanjani katika misimu yake mitatu na nusu, Madrid wameshinda 15 (65%), sare (9%) na vipigo 6 (26%).

Ukiangalia kwa karibu takwimu hizi, inakuonyesha ni kwa kiasi gani timu hiyo inamkosa mchezaji wao huyo anayeamua matokeo mara kwa mara anapokuwa hayupo. Anapocheza, Real imepoteza asilimia 11 tu ya mechi zake, ambayo ni sawa na kupoteza mechi 1 katika 10. Anapokuwa hayupo wastani huo hupanda hadi asilimia 26, zaidi ya mara mbili.

Jambo la uhakika ni kwamba ataendelea kuwabeba kwa magoli yake. Baada ya 'hat-trick' aliyoifunga katikati ya wiki kwenye Kombe la Mfalme, Cristiano sasa amefunga jumla ya mabao 175 katika mechi 172. Kwa maneno mengine, tangu awasili amefunga asilimia 39 ya magoli ya Real Madrid.

No comments:

Post a Comment