Thursday, January 17, 2013

WILSHERE AREJEA KATIKA KIWANGO AKIIVUSHA ARSENAL

Jack Wilshere wa Arsenal (10) akipongezwa na Theo Walcott baada ya kufunga goli dhidi ya Swansea wakati wa mechi yao ya Raundi ya Tatu ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 16, 2013.
Jack Wilshere wa Arsenal (katikati) akifunga goli dhidi ya beki Chico Flores wa Swansea wakati wa mechi yao ya Raundi ya Tatu ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 16, 2013.

Jack Wilshere wa Arsenal (10) akimfungisha tela Leon Britton wa Swansea wakati wa mechi yao ya Raundi ya Tatu ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 16, 2013.

Jack Wilshere wa Arsenal (kulia) akipongezwa na Olivier Giroud baada ya mechi yao ya Raundi ya Tatu ya Kombe la FA dhidi ya Swansea kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 16, 2013.
Jack Wilshere wa Arsenal (kulia) akipongezwa na Olivier Giroud baada ya mechi yao ya Raundi ya Tatu ya Kombe la FA dhidi ya Swansea kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 16, 2013.


JACK Wilshere alifunga goli la dakika za lala salama dhidi ya Swansea na kuipeleka Arsenal kwenye raundi ya nne ya Kombe la FA na sasa watawakabili Brighton.

Arsenal walipeleka presha kubwa langoni mwa Swansea katika dakika 20 za mwisho na mwisho wake wakapata goli walilostahili wakati kiungo huyo wa timu ya taifa ya England alipofunga kwa shuti la kutokea nje ya eneo la penalti.

Olivier Giroud, Theo Walcott na Thomas Vermaelen pia walikaribia kufunga lakini walibaniwa na kipa wa Swansea, Michel Vorm.

Kyle Bartley alikaribia kufunga kwa Swansea wakati kichwa chake kilipogonga 'besela'.

Nafasi hiyo ilikuwa ndiyo nzuri zaidi kwa kikosi hicho cha kocha Michael Laudrup a mbacho kilitawala kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili kilikuwa ni habari toafuti kwani Arsenal walitawala mwanzo-mwisho.

Wilshere aling'ara sana akicheza katika nafasi anayoipenda ya nyuma ya mshambuliaji.

Kiungo huyo wa England angeweza kufunga goli jingine kama kipa Vorm asingelala chini kiufundi na kuokoa mpira usiingie wavuni. Kwa ufupi, kipa huyo Mholanzi alicheza kwa kiwango cha juu akiokoa hatari nyingi, ikiwamo kuzuia shuti la Vermaelen kabla ya mapumziko na kisha kurudia ushujaa wake katika kuokoa mashuti ya Giroud na Walcott.

Shuti la Walcott la jirani na lango liliokolewa kwa kifua juu ya mstari na mshambuliaji Danny Graham, wakati krosi ya Bacary Sagna iligonga nguzo ya mbali ya lango la Vorm.

Lakini zikiwa zimesalia dakika tano mechi kumalizika, ukuta mgumu wa Swansea ulivunjwa wakati Giroud aliitumia vyema pasi ya Santi Cazorla kumtengea njiani Wilshere, ambaye alifumua shuti kutokea kwenye ukingo wa boksi na kufunga goli lake la kwanza katika Kombe la FA.

Arsenal sasa watacheza dhidi ya timu ya daraja la kwanza ya Brighton, ambayo tayari imeshaishangaza timu ya Ligi Kuu baada ya kuitoa Newcastle.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema:

"Jack alikuwa katika kiwango cha juu sana leo. Alicheza katika nafasi tofauti, mbele kidogo na ndiyo nafasi inayomfaa zaidi. Sikutegemea kama angerejea katika kiwango hiki mapema namna hii.

"Daima nimekuwa nikifikiria kwamba kama Jack atarejea katika makali yake kufikia Januari tutafanya vizuri, lakini yuko mbele ya nilichofikiria.

"Amerejea katika makali aliyokuwa nayo kabla hajaumia, nadhani hivyo, ndiyo. Kiungo aliyekamilika anaweza kusaidia ulinzi na kushambulia na Jack pia anaweza 'kuwapunguza' wapinzani na kutoa pasi za mwisho kwa wenzake."

Kocha wa Swansea, Michael Laudrup alisema:

"Tulijaribu, tukajilinda vyema, na mara nyingine kishujaa kabisa.

"Walikuwa na nafasi mbili ama tatu ambazo ungeweza kusema kwamba ni suala la muda tu watatufunga tu.

"Ungeweza kudhani kwamba mechi ingeingia katika dakika 30 za nyongeza, lakini mwishowe walistahili kushinda.

"Nataka kushinda kila mechi na wachezaji wanahitaji hilo, lakini haiwezekani kwa yeyote. Huwezi kusema sijali, inafadhaisha."



 Vikosi:


Arsenal

  • 01 Szczesny
  • 03 Sagna
  • 04 Mertesacker
  • 05 Vermaelen
  • 28 Gibbs
  • 02 Diaby (Ramsey - 82' )
  • 10 Wilshere
  • 14 Walcott
  • 19 Cazorla
  • 22 Coquelin
  • 12 Giroud

Wa akiba

  • 24 Mannone
  • 11 Santos
  • 25 Jenkinson
  • 15 Oxlade-Chamberlain
  • 16 Ramsey
  • 23 Arshavin
  • 09 Podolski

Swansea City

  • 01 Vorm
  • 02 Bartley
  • 04 Chico
  • 21 Tiendalli
  • 07 Britton
  • 12 Dyer
  • 15 Routledge
  • 20 De Guzman (Ki Sung-Yeung - 60' )
  • 26 Agustien (Pablo - 59' )
  • 29 Richards
  • 10 Graham (Michu - 71' )

Wa akiba

  • 25 Tremmel
  • 16 Monk
  • 33 Davies
  • 09 Michu
  • 11 Pablo
  • 24 Ki Sung-Yeung
  • 17 Shechter
Refa: Clattenburg
Mashabiki: 58,359


Takwimu za mechi


Possession45%55%90minsArsenalSwansea City

Mashuti

Arsenal 26  Swansea 6

Yaliyolenga lango 

Arsenal 16 Swansea 1

Kona

Arsenal 13 Swansea 3

Madhambi


Arsenal 5 Swansea 7

No comments:

Post a Comment