Robin van Magoli akishangilia baada ya kutupia |
TAKWIMU zimethibitisha kwamba Robin van Persie ameibeba sana timu yake ya Manchester United msimu huu.
Bila ya nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, Man U ingekuwa imeshinda mechi TANO tu za Ligi Kuu ya England na ingekuwa na nusu ya pointi 52 walizonazo.
Van Persie amefunga magoli 16 ya ligi na kutoa pasi sita za magoli.
Kutokana namchango wake, Man U imeshinda mechi 17, imefungwa tatu na kutoka sare moja na hivyo kuwa na wastani wa asilimia 81 za ushindi.
Lakini ukiyatoa magoli ya RVP na pasi zake za mwisho, Man U ingekuwa imeshinda mechi tano, sare 11 na vipigo vitano -- hivyo ingekuwa na wastani wa ushindi wa asilimia 23.8 tu.
Unaweza ukaiweka hivi, wakiwa na RVP, Man United wanaongoza kwa tofauti ya pointi saba juu ya mahasimu wao Manchester City kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Bila ya RVP, wangekuwa na pointi 26 na wangekuwa wakichechemea kwenye nafasi za katikati ya msimamo pamoja na klabu West Ham na Norwich.
Bwana Amur Hassan tufanyie utafiti wa Barcelona bila magoli ya Messi??
ReplyDelete