Ronaldo akitupia... |
Chezea mimi wewe? Ronaldo akishangilia 'hat-trick' yake |
Mourinho akibutua mpira kwa hasira |
Khedira akishangilia goli la nne alilofunga |
Umecheza faulo tatu, lazima uende nje... Sergio Ramos akionyeshwa kadi ya pili ya njano |
SOKA la kiwango cha juu kutoka kwa Cristiano Ronaldo liliisaidia Real Madrid kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Mfalme wakati 'hat-trick' yake ilipoiwezesha timu ya Jose Mourinho kushinda 4-0 dhidi ya Celta Vigo na kuvuka kwa jumla ya mabao 5-2. Katika mechi ya awali, Real Madrid walilala 2-1.
Huo ulikuwa ni ushindi uliogeuza historia kwani tangu mwaka 2002, Real Madrid ilishindwa kugeuza matokeo ya kutanguliwa katika mechi ya awali na kusonga mbele. Kwa miaka 10 iliyopita, Real ilikuwa ikitanguliwa katika mechi za mtoano ilikuwa ni lazima iage michuano husika na ilishashindwa katika majaribio 12.
Goli na nne lilifungwa katika dakika za lala salama na Sami Khedira wakati Sergio Ramos alitolewa kwa kadi ya njano ya pili.
Kikosi cha Mourinho sasa kitacheza dhidi ya Valencia katika robo fainali, mechi ya kwanza ikipigwa Bernabeu na ya marudiano kwenye Uwanja wa Mestalla.
Xabi Alonso alibaki katika chumba cha kuvalia baada ya mapumziko kutokana na maumivu ya mgongo. Mchezaji wa Celta, De Lucas alimuangukia Alonso shingoni na kiungo huyo hakuendelea kucheza kama tahadhari.
Mourinho alimuingiza Varane katika ulinzi, na kumpeleka mbele Essien ili asaidiane na Khedira katika kiungo.
Mourinho alikuwa mjadala tena Bernabeu. Kocha huyo alionekana kwenye hasiram, akimuwakia refa kutokana na maamuzi. Kwa hasira aliupiga teke mpira kuelekea kwenye vyumba vya kuvalia.
No comments:
Post a Comment