Lionel Messi akifurahi baada ya kupokea tuzo yake ya nne mfululizo ya Ballon d'Or ya kwenye Ukumbi wa Convention Centre mjini Zurich Uswisi leo. |
Lionel Messi akiwa kwenye tuzo za FIFA leo |
Ronaldo, Iniesta na Messi wakiwa kwenye tuzo leo |
Winga wa Fenerbahce, raia wa Slovakia, Miroslav Stoch akishukuru kwa tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka wakati wa sherehe za tuzo za FIFA Ballon d'Or leo |
Vicente del Bosque akishukuru baada ya kupokea tuzo ya Kocha Bora wa Dunia wa Mwaka 2012 |
Mwanasoka Bora wa Dunia wa zamani, Fabio Cannavaro wa Italia akionyesha jina la mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Mwaka 2012, Lionel Messi |
Straika wa timu ya taifa ya Marekani, Abby Wambach akishukuru baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa Dunia |
Mwanasoka wa zamani wa Colombia, Carlos Valderrama akisoma jina la mshindi wa tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka. |
Fuleco, kikatuni cha fainali za Kombe la Dunia 2014 za nchini Brazil kikimkumbatia mwanasoka bora wa zamani Ronaldo stejini wakati wa sherehe za tuzo za FIFA Ballon d'Or. |
Kocha wa timu ya taifa ya Brazi, Luiz Felipe Scolari na mwanasoka wa zamani wa Colombia, Carlos Valderrama wakipozi kwa picha |
Straika wa Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo na rafikiye wa kike Irina Shayk wakiingia kwenye sherehe za tuzo za FIFA Ballon d'Or. |
Rais wa FIFA, Joseph Blatter akiambatana na muigizaji wa Kirafansa, Gerard Depardieu wakati akiwasili kabla ya kuanza kwa kwenye sherehe za tuzo za FIFA Ballon d'Or. |
Waongozaji wa sherehe ya tuzo za FIFA Ballon d'Or, Ruud Gullit (kushoto) na Kay Murray wakiwa mzigoni |
NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi (25) amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya soka kutwaa tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa miaka minne mfululizo baada ya kuwashinda wapinzani wake Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Andres Iniesta wa Barcelona.
Muargentina huyo amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya miaka 61 ya tuzo hiyo kuibeba mara nne mfululizo.
Johan Cruyff (1971, 1973, 1974) na Marco Van Basten (1988, 1989, 1992) wa Uholanzi, na Michel Platini wa Ufaransa walishinda tuzo ya Ballon d'Or mara tatu.
Mwanadada Abby Wambach wa Marekani alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike, wakati tuzo ya kocha bora wa kiume ilienda kwa Vicente Del Bosque wa timu ya taifa ya Hispania baada ya kuwashinda, Jose Mourinho wa Real Madrid ambaye alishasema mapema kwamba hatahudhuria sherehe hizo nchini Uswisi na Pep Guardiola.
Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka ilienda kwa winga wa Fenerbahce, raia wa Slovakia, Miroslav Stoch ambaye alifunga goli lake kwa kuunganisha moja kwa moja bila ya kutua chini mpira wa kona uliomfikia akiwa nje ya boksi. Stoch aliwaangusha Radamel Falcao aliyefunga goli la 'tik-taka' na Neymar aliyefunga goli katika mazingira magumu.
Kikosi cha wachezaji bora "First Eleven" wa dunia chote kimeundwa na nyota wanaocheza katika Ligi Kuu ya Hispania, huku Radamel Falcao pekee akitokea nje ya Barcelona na Real Madrid.
Real Madrid na Barcelona zimetoa wachezaji watano kila moja.
Kikosi Bora cha Dunia XI cha FIFA kilichotangazwa leo ni:
Kipa
Iker Casillas
Mabeki
Dani Alves, Marcelo, Sergio Ramos na Gerard Pique
Viungo
Xabi Alonso, Xavi Hernandez na Andres Iniesta
Mastraika
Cristiano Ronaldo, Radamel Falcao na Lionel Messi
No comments:
Post a Comment