Lionel Messi wa Barcelona akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya wanaowania tuzo za FIFA za Ballon d'Or kwenye ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi Januari 7, 2013. |
Kumbe alicheka pia... Messi akifurahi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa kabla ya sherehe za tuzo |
MASHABIKI wa Cristiano Ronaldo waliachwa wakiwa hawajafurahishwa na hotuba ya kushukuru kwa ushindi wa tuzo ya Ballon d'Or iliyotolewa na nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Gazeti la Hispania la Punto Pelota limeripoti kuwa mashabiki hao hawakufurahishwa na kitendo cha Messi kutomtaja hasimu wake wa Real Madrid, Ronaldo katika hotuba yake fupi ya kushukuru kwa tuzo hiyo huku akiwashukuru "wote katika dunia ya soka isipokuwa Mreno".
Wachambuzi wa wamesema mvutano baina ya wawili hao umekuwa mkubwa kuliko ulivyokuwa katika tuzo za mwaka jana, "ungeweza kuona kwa namna walivyokuwa wakipata shida hata kutazamana" wakati wa maandalizi ya pamoja ya yale wanayotakiwa kufanya ukumbini siku ya tukio.
Wanahabari wengi pia hawakufurahishwa na tabia za Messi katika mkutano na wanahabari wa kabla ya sherehe. Ronaldo alikuwa muwazi katika majibu yake, wakati Messi alionekana kutovutiwa kuwapo hapo na alitumia muda wake mwingi akiangalia simu yake ya mkononi.
No comments:
Post a Comment