Straika wa Man City, Edin Dzeko akishangili kufunga goli la pili la timu yake dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates leo Man City walishinda 2-0. |
Huu 'mziki mnene'... Kipa wa LIverpool, Pepe Reina, akishika kichwa |
Robin van Magoli akishangilia kutupia dhidi ya Liverpool |
Chezea sisi wewe?......Van Magoli akifurahi na Evra (kushoto) na Tom Cleverley |
MANCHESTER City walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal katika mechi iliyojaa matukio kwenye Uwanja wa Emirates na kuendele kuweka presha kwa vinara Manchester United ambao mapema leo waliwatambia mahasimu wao Livepool kwa kuwapa kichapo cha 2-1.
Arsenal walibaki 10 mapema katika dakika ya 10 tu baada ya beki wao Laurent Koscielny kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumuangusha Edin Dzeko ndani ya boksi, lakini Dzeko alishuhudia penalti yake aliyoipiga katikati chini ikiokolewa na kipa wa Arsenal.
Man City walishambulia mfululizo na James Milner aliwafungia goli la kuongoza kwa shuti la kutokea pembeni katika dakika ya 21.
Dzeko alifanya matokeo yawe 2-0 katika dakika ya 32 kwa shuti la jirani na lango lakini but Arsenal walirejea wakiwa wakali kipindi cha pili kabla ya beki Vincent Kompany kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika za lala salama na hivyo timu zote kumaliza zikiwa na wachezaji 10 kila moja.
Kwenye Uwanja wa Old Trafford mapema leo, Manchester United walijiimarisha kileleni mwa msimamo kwa ushindi waliostahili wa 2-1 dhidi ya Liverpool.
Mechi hiyo ilikuwa ikitajwa kama vita ya washambuliaji Robin van Persie wa Man Ut na Luis Suarez wa Liverpool, ambao wote wako katika kiwango cha juu cha kufunga.
Na alikuwa ni Van Persie aliyetoa mchango ulioamua mechi wakati alipowafungia Man U goli tamu la kuongoza kabla ya kupiga 'fri-kiki' iliyozaa bao la pili katika dakika ya 54 wakati mpira wa kichwa wa Patrice Evra ulipomgonga Nemanja Vidic na kutinga wavuni.
Mshambuliaji aliyesajili Liverpool kwa ada uhamisho ya paundi milioni 12 kutoka Chelsea, Daniel Sturridge alifunga katika mechi yake ya pili mfululizo baada ya kuingia akitokea benchi na kuipa matumaini timu ya Brendan Rodgers na kusababisha mechi iwe na ushindani mkali katika dakika za lala salama.
Sturridge kisha akakosa nafasi nzuri ya kuwapa Liverpool pointi lakini Man U wakakomaa na kuondoka na pointi zote tatu.
Nafasi | Timu | Mechi | Goal Difference | Pointi |
---|---|---|---|---|
1. | Man Utd | 22 | 27 | 55 |
2. | Man City | 22 | 24 | 48 |
3. | Chelsea | 21 | 24 | 41 |
4. | Tottenham | 22 | 12 | 40 |
5. | Everton | 22 | 9 | 37 |
6. | Arsenal | 21 | 16 | 34 |
7. | West Brom | 22 | 1 | 33 |
8. | Liverpool | 22 | 7 | 31 |
9. | Swansea | 22 | 5 | 30 |
10. | Stoke | 22 | -3 | 29 |
11. | West Ham | 21 | -3 | 26 |
12. | Norwich | 22 | -10 | 26 |
13. | Fulham | 22 | -5 | 25 |
14. | Sunderland | 22 | -5 | 25 |
15. | Southampton | 21 | -10 | 21 |
16. | Newcastle | 22 | -12 | 21 |
17. | Wigan | 22 | -17 | 19 |
18. | Aston Villa | 22 | -25 | 19 |
19. | Reading | 22 | -16 | 16 |
20. | QPR | 22 | -19 | 14 |
No comments:
Post a Comment