Sunday, July 29, 2012

KIDUNDA ADUNDWA KIRAHISI OLIMPIKI

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kulia) akiwa hoi baada ya kudundwa kirahisi kwa pointi 20-7 dhidi ya bondia wa Moldova, Vasilii Belous katika pambano la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akishambuliwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akiendelea kuadhibiwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS

UBINGWA YANGA WAFICHUA UNAZI WA RAY, CLAUDI, CHALZ BABA, ALI KIBA, JAFFARAI ... WOTE NI YANGA KINOMAAAA!

Claudi aliwahi siti mapeeeeema uwanjani... hapa ilikuwa ni mishale ya saa saba na nusu hivi wakati AS Vita wakivaana na APR kumsaka mshindi wa tatu wa Kombe la Kagame jana 

Hawa Azam tutawafunga kweli? Claudi akionekana kama aliyejawa hofu vile... hapa ni kabla ya kuanza kwa mechi ya fainali ya timu yake ya Yanga dhidi ya Azam jana.
Dewji njoo Yanga tukupe cheo... baadhi ya wadau wa Yanga wakiwa na mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji (wa pili kulia) waliyemvuta na kukaa naye kwenye jukwaa lao wakati wa mechi dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana

Mimi niwashangilie nyie Yanga? Hapana, hilo haliwezekani... ! Mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji (wa tatu kulia) akiteta na baadhi ya wadau wa mahasimu wao Yanga wakati wa fainali ya Kombe la Kagame jana.   
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiburudika na soka safi la timu yao dhidi ya Azam jana.
Kata shingo kabisa... mtoto huyu akionyesha furaha na baba yake baada ya timu wanayoishabiki ya Yanga kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame jana.

Mtoto huyu anaendeleza mkwara wake dhidi ya wapinzani wa Yanga jana.

Muone, anashangilia kama Hamis Kiiza na Said Bahanunzi vile!
Hapa anabusu jezi ya Yanga

Anaendelea kubusu logo ya uzi wa Yanga

Msanii Vicent Kigosi 'Ray' (anayeonekana juu ya gari) akishangilia ushindi na mashabiki wenzake jana.

Ray akiendeleza shangwe na Yanga wenzake jana
Sasa ni kicheko tu... Claudi akijaidnaa kuondoka Uwanja wa Taifa baada ya kuserebuka sana na mashabiki wenzake wakati wakishangilia ushindi dhidi ya Azam. Hebu mcheki freshi, ule muonekano wa hofu kabla ya mechi uko wapi?
Chalz Baba nd'o alidatishwa kabisa kwa furaha... yeye muda wote alionekana juu ya boneti ya gari kushangilia ushindi wa chama lake.  

Yanga oyeeee! Kushoto ni Chalz Baba, kulia Ray.... wote wanashingilia ushindi na wanazi wenzao Yanga.
Mrembo huyu naye alikuwa kivutio kikubwa katika kunogesha sherehe za klabu yake ya Yanga...shavuni kajichora nini? Hayakuhusu....!

Mavuvuzela hayakutoka kirahisi mdomoni mwa mashabiki wa Yanga... si unamuona mshkaji alivyokuwa akilipuliza hadi nje ya uwanja wa Taifa baada ya Yanga kuinyamazisha Azam? Ushindi mtamu ati!

Ushindi ‘mtamu’ wa mabao 2-0 walioupata Yanga katika mechi yao ya fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya Azam jana ulifichua unazi uliopitiliza wa wasanii kadhaa nyota nchini waliofika kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi hiyo.


Baadhi ya mastaa walioonekana uwanjani hapo ili kuishangilia Yanga na kutoka kwa uwanjani kwa furaha kubwa ni waigizaji nyota Claudi na Ray, wasanii wa bongofleva Ali Kiba na Jaffarai na pia mwanamuziki Chalz Baba wa bendi ya Mashujaa.
Aliyevutia kutokana na viwalo vyake vya kiyanga-yanga zaidi ni Claudi ambaye alitupia shati la Yanga, kofia na skafu yenye rangi ya kijani na njano ya bendera ya Yanga, huku Ray, Chalz Baba na Ali Kiba wakitupia mashati na t-shirt za Yanga. 


Jaffarai aliyeketi katika jukwaa moja na Ali Kiba na Claudi hakuvaa ‘uzi’ wa Yanga pengine kutokana na hofu ya kupata kipigo kingine kama ilivyokuwa katika mechi zao nne mfululizo zilizopita ambazo zote Yanga walitoka uwanjani kichwa chini.


Hata hivyo, Jaffarai alionekana pia akijichanganya na mashabiki wenzie wa Yanga kushangilia ushindi huo mara tu baada ya kupulizwa kwa kipyenga cha mwisho, kama walivyokuwa akina Ray, Chalz Baba , Claudi na Ali Kiba.


“Nimefurahi sana… tulionyesha soka safi sana leo na kustahili ubingwa wa michuano hii,” alisema Claudi aliyekuwa amezungukwa na mashabiki kibao wa Yanga waliokuwa wakimpigia makofi na kujaribu kumbeba.
Ray na Chalz Baba waliokuwa garini, nje ya uwanja wa Taifa, pia walijikuta wakizongwa na rundo la mashabiki wenzao wa Yanga wakati wakishangilia ubingwa wa pili mfululizo wa Kombe la Kagame.


Katika mechi hiyo, washambuliaji Hamis Kiiza na Said Bahanuzi ndio waliofunga mabao ya Yanga katika kila kipindi na kuibua shangwe na vigelegele kutoka kwa maelfu ya mashabiki wao waliofika uwanjani kuiwashangilia.

NEYMAR AFANYA MAKUBWA OLD TRAFFORD

Mshambuliaji wa Brazil, Alexandre Pato (katikati) akishangilia goli lake dhidi ya kipa wa Belarus, Aleksandr Gutor (kulia) aliyelala chini huku Igor Kuzmenok akishuhudia wakati wa mechi yao ya Kundi C la michuano ya soka ya Olimpiki ya London 2012 kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester leo Julai 29, 2012. Krosi ya goli hilo ilitolewa na Neymar, ambaye pia alifunga goli moja kwa fri-kiki ya hatari iliyokwenda moja kwa moja wavuni. Brazil ilishinda 3-1. Picha: REUTERS

Mshambuliaji wa Brazil, Neymar (kulia) akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Belarus, Renan Bardini Bressan wakati wa mechi yao ya Kundi C la michuano ya Olimpiki ya London 2012 kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester Julai 29, 2012. Picha: REUTERS

SIKU ZA UCHUKUAJI FOMU VITAMBULISHO VYA TAIFA DAR ZAONGEZWA


Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu
Muda wa kujaza fomu za kuomba vitambulisho vya taifa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam sasa umeongezwa hadi Agosti 6, imefahamika.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa baada ya Agosti 6, hakutakuwa na siku nyingine zaidi zitakazoongezwa kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.

Taarifa hiyo imewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao hawajakwenda kwenye ofisi za mitaa yao ili kujaza fomu za kuomba vitambulisho vya taifa wafanye hivyo haraka, huku wageni wanaoishi nchini kihalali wakitakiwa vilevile kwenda kuchukua fomu namba mbili na kuzijaza ili kuomba vitambulisho hivyo.

Awali, zoezi la kujaza fomu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam lililoanza Julai 16 lilitakiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu.

CHICHARITO AKALIA KUTI KAVU MAN UTD

Chicharito (kulia) na Shinji Kagawa wakishiriki mazoezi ya Manchester United j\kwenye Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, Afrika Kusini Julai 17, 2012.

HATMA ya mshambuliaji Javier Hernandez 'Chicharito' klabuni Manchester United iko shakani.

Gazeti la Manchester Evening News limesema kuwa uwezekano wa kutua kwa mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie – kama Sir Alex Ferguson atafanikiwa kuwapiku mahasimu wao Manchester City katika kumsajili Mholanzi huyo – utamsukuma Chicharito nje ya nafasi za kuanza Man United.

Huku Wayne Rooney na Danny Welbeck wakiwa tayari mbele ya Mmexico huyo katika machaguo ya kocha Fergie, pia kuwasili kwa Shinji Kagawa, ambaye atatumika nyuma ya mshambuliaji mkuu, itamfanya 'Chicharito' kuachwa mbali sana katika kugombea nafasi kikosini.

BARCA: TUNAMTAKA NEYMAR BAADA YA OLIMPIKI

Neymar

Neymar wa Brazil akiwania mpira dhidi ya Joe Allen wa timu ya Great Britain wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough, England Julai 20, 2012.
Neymar akifanya mambo yake...

Neymar wa Brazil akishangilia kufunga penalti dhidi ya timu ya Great Britain wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough, England Julai 20, 2012.

MAKAMU wa rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu ametangaza kuwa klabu hiyo inataka kumsajili nyota wa Santos, Neymar katika kipindi hiki cha usajili.

Bartomeu amebainisha kuwa wanayo matumaini ya kumpata mshambuliaji huyo mwenye kipaji wa Brazil baada ya fainali za Olimpiki zinazoendelea London.

"Sote tungependa Neymar aje hapa baada ya Olimpiki," Bartomeu aliripotiwa kuwaambia mashabiki wa Barca nchini Morocco ambako usiku wa jana Barcelona ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Raja Casablanca ya huko.

"Yeye ni mchezaji wa Santos (kwa sasa) lakini nina hakika Neymar atakuja Ulaya baadaye, na wakati huo utakapowadia tutakuwa makini ili ajiunge na Barcelona."

VAN PERSIE ATAKA MSHAHARA WA ROONEY ATUE MAN UTD

Robin van Persie

MUASI wa Arsenal, Robin van Persie anataka kuwa mshahara sawa na wa Wayne Rooney kama Manchester United wanataka ajiunge nao.

Gazeti la Daily Star Sunday limesema kuwa Van Persie atajiunga na Man United kama ataahidiwa mshahara mkubwa kama wa Rooney.

Nyota wa timu ya taifa ya England, Rooney ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni Man United ambao ni paundi 220,000 (sawa na Sh. milioni 537) kwa wiki na mshambuliaji wa Arsenal, RVP anataka mshahara kama huo.


MTAZAME LIONEL MESSI ANAVYOKULAGA BATA NA MREMBO WAKE ANTONELLA....... NI BALAAAAAA!

Pendedhaaa eeenh....! Messi na mpenzi wake aliye mjamzito kwa sasa, Antonella Roccuzzo, wakiwasili katika eneo la mnuso wa harusi ya Iniesta hivi karibuni.

Mshumu tena...! Messi na demu wake Antonella Roccuzzo wakijiachia ufukweni.

Messi na mepnzi wake Antonella Roccuzzo kwa mbwembwe nd'o wenyewe.... Eti hapa wanajifanya wamesusa!
Mnaangalia nini? Messi akiendelea kujiachia ufukweni na mpenziwe Antonella Roccuzzo 

Mmmhh... ni raha tupu. Hapa Messi na demu wake Antonella Roccuzzo wakiponda maraha ndani ya boti ya kifahari

Hapa Meesi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo wakiwa ndani ya boti ya kifahari

Ni kujiachia ufukweni kwa kwenda mbele.... hapa Messi na mpenzi wake Antonella sijui walikuwa Coco Beach?

Duh...ni fulu kujiachia. Hapa ni wakati Antonella akiwa mapumzikoni na Messi ndani ya boti ya kifahari, siku chache kabla hajashika ujauzito. 

Sijui turudi tena ndani ya boti? Hapa Messi na Antonella wakijianika juani baada ya kuogelea weee hadi wakatepeta kwa uchovu.

Sasa akaunti yetu ina mihela kibao... soka linalipa bwana. Kwanini tusitafute mtoto kama wa Cristiano Ronaldo? Pengine ndivyo Antonella na Messi wanavyoambiana wakati wakiendelea kula bata ufukweni.

Soma meseji hii... Messi na Antonella wake wakiendelea kuponda maraha baada ya msimu wa ligi kumalizika.
Messi sio tu anacheza soka, bali anapenda soka... hii ilikuwa mwezi uliopita wakati akijiachia kwenye fukwe za Miami, Marekani.

Messi akiwa na kibukta chake cha ufukweni wakati akiwa mapumzikoni Miami, Marekani.

Messi na washkaji zake wakifaidi maisha kwenye fukwe za Miami, Marekani mwezi uliopita

Messi na mpenzi wake Antonella wakikatiza mitaa. Hapa ni kabla Antonella hajashika ujauzito.

Sijui ntapata mtoto wa kiume kama Cristiano Ronaldo? Hapa Messi akisinzia baada ya kuchezea sana maji kwenye fukwe za Miami, Marekani mwezi uliopita.


Messi na demu wake Antonella wakikatiza katika mitaa ya ufukweni walikoenda kufaidi samaki-samaki.

Ya nini tabu wakati raha ziko tele duniani? Messi, demu wake Antonella na wapambe wakiendelea kujiachia ufukweni.
Messi, demu wake Antonella na wapambe zao wakianza safari ya kwenda kuvua samaki... ni raha juu ya utamu!

Huyu ndiye Antonella, kimwana anayemuondolea upweke Lionel Messina kumsaidia katika kutumia mabilioni ya fedha anayoingiza kila mwaka na kuwapita wanasoka wote duniani.

Twende mpenzi... Messi na demu wake Antonella wakiwa ufukweni.

Antonella akiwa katika pozi lake linalomtuliza Messi... hapa jini Messi hafurukuti, chenga zake, magoli yake ya kichawi na kasi yake ya umeme awapo uwanjani huishia hukooooo.... sio mbele ya  kimwana huyu ati!




Nani kasema Lionel Messi mpole? Basi ukimtaka ugomvi ni rahisi sana... mguse huyu kimwana wake Antonella. Kama hajakutoa manundu kachinje mende!

Mrembo Antonella Roccuzzo ndiye tulizo la roho la Lionel Messi, nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.

Kwa muda mrefu sasa, Messi na Antonella wamekuwa wakiambatana kwenye viwanja vya kuponda maraha, wakihama kutoka fukwe moja na kwenda sehemu nyingine ya kujidai, hasa nyakati ambazo Messi huwa 'free' baada ya kumalizika kwa msimu wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

Hivi sasa, penzi la wapendanao hawa limenoga kwelikweli na Messi alishatangaza tangu mwezi uliopita kwamba wako mbioni kupata mtoto wake wao wa kwanza.

"Najua atakuwa ni mtoto wa kike," alikaririwa Muargentina Messi, ambaye ni mshindi mara tatu mfululizo wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia.

"Sitaki kueleza zaidi kwa sababu huwa hatupendi kuzungumzia maisha yetu binafsi, lakini hilo limeshathibitika na kuleta furaha kwa familia yangu na familia yao (Antonella). Tunasubiri kwa hamu siku hiyo ya kupata mtoto," mchezaji huyo nyota wa Barcelona alikaririwa akisema.