Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu |
Muda wa kujaza fomu za kuomba vitambulisho vya taifa kwa wakazi
wa jiji la Dar es Salaam sasa umeongezwa hadi Agosti 6, imefahamika.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa baada ya Agosti 6, hakutakuwa na
siku nyingine zaidi zitakazoongezwa kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.
Taarifa hiyo imewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao
hawajakwenda kwenye ofisi za mitaa yao ili kujaza fomu za kuomba vitambulisho
vya taifa wafanye hivyo haraka, huku wageni wanaoishi nchini kihalali
wakitakiwa vilevile kwenda kuchukua fomu namba mbili na kuzijaza ili kuomba
vitambulisho hivyo.
Awali, zoezi la kujaza fomu kwa wakazi wa jiji la Dar es
Salaam lililoanza Julai 16 lilitakiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment