Jose Bosingwa |
Harry Redknapp |
KOCHA wa QPR, Harry Redknapp amekiri kwamba kuna mambo "yanamsumbua" tangu alipotua kuifundisha klabu hiyo.
Redknapp alimshuhudia beki wa kulia Jose Bosingwa akiondoka kwa hasira kutoka katika chumba cha kuvalia baada ya kuambiwa kwamba hatakuwamo katika kikosi cha kwanza na akakataa kukaa benchi kwa ajili ya mechi yao ya wikiendi iliyopita dhidi ya Fulham.
Kocha huyo hajafurahishwa na kitendo cha beki huyo wa zamani wa Chelsea ambaye anajiona ni bora sana kiasi kwamba hastahili kukaa benchi huku pia akisema baadhi ya wachezaji klabuni hapo wanajiona ni zaidi ya wengine.
"Inanisumbua pale mchezaji anapokataa kukaa benchi wakati mnapokuwa matatizoni," alisema.
"Sote tuko matatizoni. Mmiliki na mashabiki wanaona timu yao inafungwa kila wiki na mara unakuta mtu hataki kukaa benchi.
"Yeye (Bosingwa) alisema: 'Sitaki kukaa benchi.' Anadhani kwamba yeye ni bora sana hivyo hastahili kukaa benchi. Hilo ndilo linalonisumbua katika mchezo huu.
"Nimeshuhudia tukio moja ama mawili ambayo yananisumbua."
Redknapp alisema hana uhakika kama atampanga tena Bosingwa: "Nitalazimika kuliangalia suala hilo huko mbele. Ngoja tuone tunaendaje."
No comments:
Post a Comment