TIMU inayochechemea katika ligi ya mchezo wa American Football ya New York Jets huenda ikawa imepata 'supastaa' mpya.
Video ya kijana aitwaye Havard Rugland inayomuonyesha akiupiga mpira wa mchezo huo kwa shabaha ya ajabu tena katika umbali mrefu, kwa 'tik-taka' na hata kulenga vitu vinavyotembea, imempa umaarufu mkubwa kiasi kwamba amechukuliwa na klabu hiyo kwa ajili ya kufanyiwa majaribio ya kujiunga nayo.
Rugland, ambaye anatokea Aalgaard, Norway, alianza kupiga mpira huo miaka miwili tu iliyopita, lakini shabaha yake — hata katika gari linalotembea — imeonekana na kuaminiwa.
"Havard ana kipaji cha ajabu cha kupiga mpira," kocha wa Jets, Michael Husted alisema.
Na wakati kukiwa bado hakuna tamko lolote kama timu hiyo ya Jets itampa mkataba kijana huyo mwenye umri wa miaka 27, Rugland alikiambia kipindi cha Good Morning America anaamini kwamba majaribio yake ya kujiunga na timu hiyo "yameenda vyema".
No comments:
Post a Comment