Kikosi bora cha 2012 katika mfumo wa 4-3-3 |
WATUMIAJI wa internet wapatao 70,000 wamepiga kura katika utafiti uliofanywa na tovuti ya Hispania uliolenga kupendekeza 'First Eleven' ya mwaka 2012 duniani, ambapo takribani wachezaji wote walioingia katika kikosi hicho wanacheza katika Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).
Wachezaji watano wa kikosi hicho wanatokea Barcelona, wanne Real Madrid, mmoja Radamel Falcao anatokea Atletico na mchezaji pekee anayetokea nje ya ligi ya Hispania ni Philipp Lahm wa Bayern Munich.
Katika kura zilizopigwa, nafasi ya golikipa ilichukuliwa na Iker Casillas aliyeongoza kwa kupata kura nyingi zaidi ya wachezaji wote ambapo alipata asilimia 74.6 akimzidi Manuel Neuer (Bayern) aliyepata 12% ambaye kwa maana hiyo atakuwa kipa wa akiba.
Kikosi hicho kimeteuliwa kwa mfumo wa 4-3-3, ambapo nafasi ya mabeki wanne inaundwa na Lahm (10.9%), Gerard Pique (12.5%), Jordi Alba (19%) na beki aliyepata kura nyingi zaidi, Sergio Ramos (20,2%). Beki wa Borussia Dortmund, Matt Hummels (8.1%) na wa Real Madrid, Pepe (7.6%) watasubiri benchi.
Viungo waliochaguliwa ni Xabi Alonso (11.8%) kama kiungo wa ulinzi na Xavi (22.4%) na Iniesta (29.5%) ambao wanakamilisha safu ya viungo watatu. Andrea Pirlo wa Juventus aliyepata asilimia 10% na David Silva wa Man City (9.4%) watakuwa wachezaji wa akiba.
Kwenye safu ya ushambuliaji ndipo mahala palipotisha zaidi ambapo wameteuliwa mastraika watatu wanaotisha zaidi kwa kufumania nyavu katika sayari hii: Lionel Messi aliyepata kura asilimia 30.3, Falcao (27.4%) na Cristiano Ronaldo (20.3%) huku Zlatan Ibrahimovic wa PSG aliyepata asilimia 7 na Robin Van Persie wa Man United aliyepata asilimia 4.7 wakisubiri.
No comments:
Post a Comment