Anaendelea kumpasha... Anayoyasema hapa Fergie weka mwenyewe..... |
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson hataadhibiwa kwa kumbwatukia refa Mike Dean kwenye Uwanja wa Old Trafford katika mechi dhidi ya Newcastle, chama cha soka England (FA) kimethibitisha.
Ferguson alimfuata Dean wakati wakitoka vyumbani kwa ajili ya kuanza kipindi cha pili, kabla ya kuwafuata mwamuzi wa akiba Neil Swarbrick na Jake Collin.
FA imethibitisha leo kwamba hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi ya kocha huyo kwa sababu Dean hakuandika kwenye ripoti yake kwamba alifuatwa na Ferguson.
No comments:
Post a Comment