Wednesday, November 21, 2012

BONDIA BINGWA WA ZAMANI WA DUNIA APIGWA RISASI NDANI YA GARI

Hector ''Macho'' Camacho
Hector ''Macho'' Camacho
Hector ''Macho'' Camacho

Hector ''Macho'' Camacho akipatiwa msaada baada ya kupigwa risasi

Hector ''Macho'' Camacho
Hector ''Macho'' Camacho akipatiwa msaada baada ya kupigwa risasi


SAN JUAN, Puerto Rico
BINGWA wa ndondi wa dunia wa zamani Hector ''Macho'' Camacho amejeruhiwa vibaya katika shambulio la risasi nje ya mji mkuu wa Puerto Rico jana Jumanne, na madaktari na msemaji wake wamesema anatarajiwa kupona.

Mtu mmoja aliwafyatulia risasi Camacho (50) na mtu mwingine wakiwa wamekaa kwenye gari katika mji wa Bayamon. Mtu mwingine ambaye uhusiano wake na bondia huyo wa zamani haujafahamika, aliuawa, kwa mujibu wa taarifa ya polisi. Mtuhumiwa wa shambulio hilo anashikiliwa na polisi.

Camacho alikimbizwa katika hospitali ya Centro Medico ya mjini San Juan, ambapo alikuwa katika hali mbaya lakini akiwa mzima, Dk. Ernesto Torres, mkurugenzi wa hospitali hiyo, aliwaambia waandishi wa habari.

Risasi hiyo ilimpiga kwenye taya lakini ilitoka kichwani na kunasa kwenye bega lake la kulia, Torres alisema. Daktari huyo alisema Camacho, ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya utumiaji wa dawa za kulevya na ulevi wakati akiwa bondia, yuko hatarini kupooza kutokana na risasi hizo.

Wakala wa Camacho, Steve Tannenbaum alisema ameelezwa na marafiki zake hospitalini hapo kuwa bondia huyo atapona. 'Mtu huyu ni paka mwenye roho tisa. Amepitia mengi sana,'' alisema. 'Kama yuko yeyote atakayepona basi atakuwa ni yeye.''

Pambano la mwisho la ubingwa la bondia huyo lilikuwa ni dhidi ya bingwa wakati huo wa uzioto wa welterweight, Oscar De La Hoya mwaka 1997, ambapo alipigwa kwa pointi. Tannenbaum alisema Camacho alitarajia kupambana nchini Denmark miaka miwili iliyiopita lakini mpinzani wake alijitoa na walikuwa wakisaka pambano la mwaka 2013.

''Tulikuwa tukizungumzia kurejea kwake licha ya kwamba ana miaka 50,'' alisema. ''Niliona kwamba anaweza kupambana.''

Camacho alizaliwa Bayamon. Alitwaa ubingwa dunia wa ndondi katika uzani super lightweight, lightweight na junior welterweight katika miaka ya '80.

Bondia Camacho alipambana mapambano makubwa dhidi ya mabondia kama Felix Trinidad, Julio Cesar Chavez na Sugar Ray Leonard. Camacho alimpiga kwa KO Leonard mwaka 1997, na kuzima jaribio la bingwa huyo wa zamani wa dunia la kutaka kurejea mchezoni.

Camacho ana rekodi ya 79-5-3, huku mapambano yake mengi yakija mwaka 2009.

Dawa za kulevya, pombe na matatizo mengine yalimuandama Camacho tangu kuwa maarufu katika ngumi. Alihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani mwaka 2007 kwa kuiba katika stoo ya kompyuta mjini Mississippi. Wakati akikamatwa kwa mashitaka hayo ya wizi Januari 2005, polisi pia walimkuta na kete ya "unga".

Jaji, hata hivyo, aligeuza kifungo hicho kuwa cha nje Camacho. Akaja kukaa gerezani wiki mbili kwa kukiuka masharti ya kifungo hicho cha nje.

Mara mbili mkewe alifungua mashitaka ya kupigwa, na akafungua madai ya talaka miaka kadhaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment