MADRID, Hispania
JERAHA la kuteguka kiwiko cha mkono litamuweka Carles
Puyol nje ya uwanja kwa takriban miezi miwili na hiyo inamaanisha kuwa kocha
Tito Vilanova wa Barcelona atakabiliwa na tatizo jingine la ulinzi wa kati
katika mechi yao ya 'Clasico' kwenye La Liga, Ligi Kuu ya Hispanai dhidi ya
Real Madrid Jumapili.
Katika mechi yake ya kwanza tangu apone jeraha la goti,
Puyol alianguka vibaya kipindi cha pili katika ushindi wao wa 2-0 wa mechi ya
Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica na klabu yake imesema
kuwa atakuwa nje kwa takriban wiki nane.
No comments:
Post a Comment