![]() |
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Liberatus Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
Polisi wakiwa na jeneza la mwili wa marehemu Kamanda Barlwo kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
![]() |
Baadhi ya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
![]() |
Gari lililobeba mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
Waziri William Lukuvi akitoa heshima zake za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
![]() |
Waombolezaji wakiendelea kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
![]() |
Kwaheri Kamanda Barlow...! |
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndikilo akihutubia waombolezaji wakati wa kuuaga mwili wa Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
![]() |
DCI Manumba (wa pili kutioka kulia, mbele) akiwa katika shughuli ya kuuaga mwili wa Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. |
![]() |
Mwalimu Dorothy Moses, aliyekuwa na marehemu wakati wa tukio |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliojitokeza leo kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kuuaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Liberatus Barlow aliyeuawa usiku wa kuamkia juzi Jumamosi kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
Mamia
ya wananchi walihudhuria kuagwa kwa mwili wa kamanda huyo ambao ulisafirishwa
kwa ndege jioni hii kuelekea jijini Dar es.
Waziri
Lukuvi alisema kuwa Jeshi la Polisi liko imara na kwamba makamanda wengine wataendeleza
jitihada za marehemu (Kamanda Barlow) katika kupambana na uhalifu bila kuchoka.
Kwa
mujibu wa ratiba, mwili wa Kmanda Barlow jijini Dar es Salaam kesho saa tano
asubuhi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Augustine Ukonga kabla ya kwenda
kuzikwa nyumbani kwao, Vunjo mkoani
Kilimanjaro.
DCI
ROBERT MANUMBA
Akizungumza
katika shughuli kuuaga mwili huo jijini Mwanza leo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai, DCI Robert Manumba, alisema kuwa hadi sasa wamefikia hatua
nzuri katika upelelezi wao kutokana na ushirikiano wanaupata kwa wananchi na
kwamba wauaji ni lazima watapatikana.
Wengine
waliozungumza mbele ya waombolezaji ni
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,
Phillip Kalangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Salum Msangi, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Geita, Lenard Paul na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Anthony
Ruta.
Kamanda
Barlow aliuawa usiku wa kuamkia juzi (Jumamosi) kwa kupigwa risasi usiku wa kuelekea
saa 8:00 baada ya kumfikisha mwanamke aliyempa lifti kwenye gari yake binafsi baada
ya kumalizika kwa kikao cha harusi, Mwalimu Doroth.
Rais
Jakaya Kikwete ametuma salam za rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspeka
Jenerali Saidi Mwema, kuhusiana na kifo cha Kamanda Barlow na kuagiza jeshi
hilo kuwakamata wahusika na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria.
No comments:
Post a Comment