Chicharito |
Real Madrid wameanza kumfuatilia kwa karibu straika Javier Hernandez ambaye hana uhakika wa namba katika klabu yake ya Manchester United.
Chicharito amejikuta akiwekwa benchi muda mwingi msimu huu baada ya kuwasili kwa Robin van Persie na kuimarika kwa Danny Welbeck. Pia ujio wa straika kutoka Chile, Angelo Henriquez.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ni shabiki mkubwa wa Chicharito na anaamini kuwa ujio wa nyota huyo wa Mexico utawapa mafanikio makubwa.
Hata hivyo, Chicharito amesisitiza kuwa anafurahia maisha katika klabu yake ya Man U.
No comments:
Post a Comment