Friday, September 7, 2012

RONALDO NI "SHARO" SANA - ROONEY

Rooney akimpongeza Ronaldo wakati wakiwa pamoja Manchester United
Rooney (kushoto) akimpongeza Ronaldo wakati wakiwa pamoja Manchester United
Rooney na Ronaldo wakipongezana wakati wakiwa pamoja na Manchester United.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akiwasili na wachezaji wenzake kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu huu dhidi ya  Los Angeles Galaxy katika Uwanja wa Rose Bowl mjini Pasadena, California, Marekani Agosti 7, 2010.


Marcelo (kushoto) na Cristiano Ronaldo (wa pili kushoto), wa Real Madrid wakimpongeza mchezaji wa timu ya vijana aliyeshiriki mazoezi katika mazoezi yao baada ya kufunga goli Agosti 5, 2010 Westwood, Los Angeles, California.
Rooney (kushoto) akitaniana na Ronaldo mazoezini enzi wakiwa pamoja Manchester United

WAYNE Rooney amesema mchezaji mwenzake wa zamani Manchester United,Cristiano Ronaldo ni "sharobaro" sana kiasi kwamba hawezi kukipita kioo bila ya kujiangalia!

Rooney amemzungumzia nyota huyo wa Real Madrid katika kitabu chake kipya kiitwacho "Miaka Yangu 10 Katika Ligi Kuu ya England na Wayne Rooney", ambacho kinachapishwa mfululizo katika gazeti la Mirror.

"Kulikuwa na kioo kwenye kiti cha Cristiano Ronaldo katika chumba cha kuvalia cha Old Trafford.

"Katika wakati niliokuwa nikicheza soka na Ronnie, jambo moja nililobaini kuhusu yeye ni kwamba hawezi kupita kioo bila ya kujicheki, hata kama tunakaribia kuanza mechi.

"Kila mechi, kabla ya timu haijatoka kwenda kupasha, anafanya jambo hilo hilo. Anavaa jezi, viatu. Na muda mfupi baadaye, Ronnie anajiangalia kwenye kioo.

"Kama kuna mtu anayejiamini kuliko Ronaldo basi sijawahi kukutana naye. Haoni aibu.

"Anapenda nguo zake na "kufuli" analovaa daima huwa ni la bei kali lenye jina la wabunifu wakubwa – Dolce & Gabbana, Armani, mnayajua, ana swagga zake wakati akiingia kwenye uwanja wa mazoezi, anapenda kupendeza kuanzia kichwani hadi mguuni.

"Lazima atakuwa anatumia pesa nyingi kwa ajili ya mavazi yake. Lakini mapenzi makubwa zaidi ya Ronaldo yako kwenye soka.

"Kwenye uwanja wa mazoezi hutuambia anataka kuwa mchezaji bora wa dunia, hilo ndilo jambo kubwa analotaka, kuwa gwiji.

"Ana malengo ya kufanikisha jambo hilo. Kwa uwazi, napenda tabia yake hiyo, lakini haiko hivyo kwangu.

"Mimi napenda zaidi kuisaidia timu kutwaa mataji mengi kuliko kupata tuzo binafsi za kwenda nazo nyumbani.

"Lakini kama Ronnie anataka kuwa manasoka bora duniani na ikaisaidia United kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu wa kwanza tangu mimi kutua katika klabu hii, basi safi, naikubali."

No comments:

Post a Comment