Wednesday, September 5, 2012

MO FARAH AJIPIGIA DEBE ARSENAL, FULL KUMUIGA BOLT

Mo Farah wa Uingereza akishangilia kwa staili yake aliyobuni ya kuweka mikono miwili kichwani baada ya mbio za mita Maili 2 wakati wa mashindano ya riadha ya Samsung Diamond League 2012 Aviva Birmingham Grand Prix kwenye Uwanja wa Alexander mjini Birmingham, England Agosti 26, 2012.
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt akishangilia kwa staili yake maarufu ya "flying guitar"
Mo Farah (kushoto) akipozi kwa staili ya kushangilia ya Usain Bolt, huku Bolt (kulia) naye akipozi kwa staili ya Mo Farah

MSHINDI wa tuzo mbili za dhahabu katika Olimpiki, Mo Farah ameonyesha ni shabiki mkubwa wa Usain Bolt na kila anachofanya Bolt naye ni 'full' kumuiga.

Mo Farah, Muingereza mwenye asili ya Somalia, ameiomba klabu anayoishabiki ya Arsenal imsajili kama kocha wa 'fitness' atakapostaafu kazi yake ya riadha. 

Bingwa wa dunia wa riadha wa mita 100, Usain Bolt anafahamika kwa mapenzi yake kwa klabu ya Manchester United na amewaomba mashabiki wampigie debe kwa kocha Alex Ferguson amsajili.

Farah pia naye amebuni staili yake ya kushangilia (muangalie pichani) kufuatia umaarufu mkubwa wa staili ya kushangilia ya Bolt.

No comments:

Post a Comment