Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Happines Millen Magese akishiriki Wiki ya Mitindo ya Mavazi ya New York nchini Marekani jana. Onyesho hilo lilishuhudiwa na nyota wakubwa kama mwanasoka David Beckham huku wabunifu wakubwa duniani wakishiriki kuonyesha mitindo yao ya mavazi kama Tommy Hilfiger, Carolina Herrera, Michael Kors, Ralph Lauren na mwanamama Tracy Reese, ambaye gauni lake lilivaliwa na mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama katika Kongamano la Kitaifa Chama cha Democratic. Mwanamitindo maarufu Naomi Campbell pia alipita stejini kuonyesha mitindo. Picha: REUTERS |
No comments:
Post a Comment