Friday, September 7, 2012

DJ WA CHRIS BROWN AZUNGUMZIA JIJINI DAR LEO BUSU LA BREEZY NA RIHANNA KWENYE TUZO ZA MTV JANA USIKU

Rihanna (kushoto) akibusiana na boifrendi wake wa zamani Chris Brown (kulia) wakati wa tamasha la tuzo za video bora za muziki  la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.
Rihanna (kushoto) na rapa A$AP Rocky wakitumbuiza stejini wakati wa tamasha la tuzo za video bora za muziki  la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.
Rihanna akitumbuiza stejini wakati wa tamasha la tuzo za video bora za muziki  la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.
Rihanna akitumbuiza stejini wakati wa tamasha la tuzo za video bora za muziki  la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.
Rihanna akishukuru kwa tuzo ya Video Bora ya Mwaka wakati wa tamasha la tuzo za video bora za muziki  la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.

Rihanna akiwasili kwa ajili ya tamasha la tuzo za video bora za muziki la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.

Rapa Wiz Khalifa (kushoto) akishika tumbo la mchumba wake mwanamitindo Amber Rose wakati wakiwasili kwa ajili ya tamasha la tuzo za video bora za muziki la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.

Rapa Wiz Khalifa (kushoto) akiwasili na mchumba wake mwanamitindo Amber Rose kwa ajili ya tamasha la tuzo za video bora za muziki la MTV Video Music Awards 12 kwenye Ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California jana usiku Septemba 6, 2012.
Amber Rose akionyesha tumbo la ujauzito wa mchumba wake rapa Wiz Khalifa na kuthibitisha uvumi uliozaga kwamba mwanamitindo huyo anatarajia mtoto wake wa kwanza 

DJ wa Chris Brown, DJ Babey Drew, ambaye yuko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupagawisha mashabiki kesho Jumamosi kwenye Ukumbi wa Savanna Lounge, amemtetea bosi wake kwamba hajarejesha mahusiano na Rihanna licha ya wawili hao kubusiana wakati wa tamasha la tuzo za video za muziki la MTV Video Music Awards 2012 jana usiku.
 
Rihanna alimbusu boifrendi wake wa zamani Chris Brown ukumbini wakati wa tamasha hilo la tuzo kwenye ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles, California na kuzua mijadala mipya kwamba huenda wawili hao wamerudiana ama wako mbioni kurudiana. 

Kamera za televisheni zilikosa tukio hilo kubwa wakati Rihanna na Chris Brown walipokumbatiana na kubusiana, lakini mtu mmoja alitoa kamera ya simu yake na kupiga picha.

Vyanzo vilivyo karibu na Rihanna vilisema kuwa wawili hao walikuwa wakiandikiana meseji kwa muda wote wa usiku.

"Walikuja katika tuzo kupima maji, wanapendana sana," chanzo kilisema.

"Walikuwa wanaandikiana meseji na kupongezana kwa shoo zao walizofanya stejini."

Chanzo kilisema Rihanna ndiye aliyemshawishi Chris Brown kuhudhuria tamasha hilo.

Rihanna alishinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, wakati Chris Brown alitwaa tuzo ya Video Bora ya Msanii wa Kiume.

Hata hivyo, Dj Babey Drew, amemwambia mtangazaji Dj Fettie wa kipindi cha XXL cha radio Clouds FM katika studio hiyo jijini Dar es Salaam leo kuwa wawili hao ni marafiki tu.

"Ina maana hujaona mapicha yanayowaonyesha wanavyobusiana?" aliuliza Fettie kumwelekeza swali DJ huyo wa Chris Brown.

"Inawezekana amem-kiss kidevuni," alisema DJ huyo raia wa Jamaica, ambaye pia ni mtangazaji wa radio.

DJ huyo amesema amekuwa akifanya kazi ya U-DJ katika shoo zote za Chris Brown.

Kiingilio cha katika shoo ya Savanna kesho kimetangazwa kuwa ni  Sh. 25,000.

No comments:

Post a Comment