Wednesday, September 5, 2012

BONITE YAWAZADIA WASHINDI PROMOSHENI YA VUTA MKWANJA

Meneja Masoko wa Bonite Bottlers, Christopher Loiruk (kulia) akimkabidhi fedha taslimu mshindi wa promosheni ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola, Rahim Hassan zawadi ya Sh. milioni 1wakati wa hafla ya makabidhiano  kwenye makao makuu ya Bonite Bottlers mjini Moshi.

Hamida Nkya, mkazi wa Arusha na mshindi wa Sh. milioni 1 ya Promosheni ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola, akizungumza baada ya kukabidhiwa malipo yake taslimu kwenye makao makuu ya  Bonite Bottlers mjini Moshi.

KAMPUNI ya vinywaji baridi jamii ya Coca-Cola ya Bonite leo imewazawadia fedha taslimu washindi wengine 16 wa promosheni ya Vuta Mkwanja ambayo ilianza mwezi Julai na inatarajiwa kufikia tamati mwezi huu.

Washindi hao ni Fredy Charles mkazi wa Mianzini, Arusha, Hamid Nkya (Ngaramtoni Arusha) na Rahim Hashim (Majengo, Moshi) ambao kila mmoja amejishindia zawadi ya pesa taslimu Sh. milioni 1. Fedha hizo wamekabidhiwa leo kwenye makao makuu ya Bonite Bottlers mjini Moshi.


Waliobahatika kujishindia Sh. laki moja ni Goodluck Kessy (KCMC – Kitandu), Focus Njau (Uchira, Moshi), Joseph Kauwedi (Lyamungo Sec, Moshi), Samson Mushi (Kiusa, Moshi), Fatuma Ibrahim (Babati), Narender Mushi (Moshi Town).


Wengine ni Julius Michael (Sakina, Arusha), Christina Kessy (Arusha), Dorin Massawe (Arusha), Khadija Said (Kijenge – Arusha), Lucas Tito Sumari (Makumira), Magdalena John (Kimandolu – Arusha) na Lilian Maro (Ngaramtoni – Arusha).


Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi yake, mmoja ya washindi wa Sh. milioni 1, Hamida Nkya (41) ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari ya Mlinga iliyopo Ngaramtoni, Arusha, alisema anajisikia furaha sana kupata bahati ya kuwa mshindi.


"Siku ya leo ninayo furaha sana, nilikunywa soda ya Fanta nikaangalia chini ya kizibo nikakuta nimejishindia Sh. milioni 1. Nilikuwa na ndoto ya siku nyingi ya kuanzisha mradi wa kufuga kuku na tatizo ilikuwa ni mtaji. Ni kama ndoto imekuwa ya ukweli. Natoa shukrani kwa Mungu kwani riziki anatoa yeye. Napenda kuipongeza Kampuni ya Bonite Bottlers kwa promosheni hii ambayo kweli itabadilisha maisha yangu," aliongeza Nkya.


Dorin Massawe (19), muuza duka wa Jijini Arusha na mshindi wa Sh.100,000 alisema alikunywa soda ya Fanta Passion na kubahatika kuwa mshindi. "Nilikuwa siamini watu waliposema kuwa kwa kunywa soda za jamii ya Coca-Cola unaweza kushinda. Nashukuru leo nimeamini kwa macho yangu," alisema Dorin.


Akiongea wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa Bonite Bottlers, Christopher Loiruk alitoa wito kwa wateja wa Coca-Cola kuendelea kunywa sod za Coca-Cola pamoja na jamii hiyo na kuibuka washindi.


"Kuna washindi ambao wamejishindia zawadi mbali mbali kwa kunywa soda za Coca-Cola, Fanta na Sprite. Soda yeyote ya jamii ya Coca-Cola unayokunywa una nafasi ya kuwa mshindi," anaongeza Loiruk.


Promosheni hii imewawezesha wateja wengi wa Bonite Bottlers kujishindia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sh. milioni 1, Sh. 100,000, Sh. 10,000, Sh 5,000, Sh. 2,000, fulana za Coca-Cola na soda za bure.

No comments:

Post a Comment