Cristiano Ronaldo |
LOS ANGELES, Marekani
STRAIKA Cristiano Ronaldo amesema kuwa amefurahia tuzo aliyopata
ya kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia inayiandaliwa na mtandao maarufu wa soka
wa Goal.com, huku akiongeza kwamba anajisikia fahari kupewa heshima hiyo.
Baada ya mazoezi ya Real Madrid jana
jioni jijini Los Angeles, nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alikutana na waandaaji
Goal.com na kutoa shukrani zake kwa kuchaguliwa kuwa kinara miongoni mwa wachezaji
hamsini waliopigiwa kura, akiwamo hasimu wake Lionel Messi ambaye ndiye Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia wa FIFA.
“Ni suala la kujivunia kwangu baada ya
kuwa mshindi wa tuzo hii," alisema mshindi huyo ambaye hii ni mara yake ya pili kutwaa tuzo hiyo ya ‘Wanasoka
nyota 50 wa Goal.com’.
"Nisingeweza kupata mafanikio
haya bila kusaidiwa na wachezaji wenzangu,” aliongeza Ronaldo.
Ronaldo pia alisaidia wenzake kwa kutoa
pasi 15 za magoli, hivyo kuwa mmoja wa vinara wa timu yake kwa kutoa pasi za mabao.
Tangu kutua kwa kocha Jose Mourinho
mwaka 2011, Cristiano Ronaldo na Real Madrid wametwaa Kombe la Mfalme na La
Liga.
“Malengo yangu kwa sasa ni kucheza kwa
juhudi na wenzangu ili kutwaa mataji katika kila michuano itakayokuwa mbele
yetu. Sikusudii kombe moja kwa sababu nataka tupiganie kila taji, lakini ili
kufanikiwa, tunapaswa kupambana kwa
nguvu zetu zote," mshambuliaji huyo aliongeza.
"Naamini kwamba kwa timu kali
kama yetu, hakutakuwa na vikwazo vya kutisha mbele yetu,” alisema Ronaldo.
Cristiano Ronaldo alikuwa mhimili wa mafanikio ya
Real Madrid msimu uliopita, akifunga mabao 46 katika mechi zote 38 za ligi
alizocheza wakati wakiipoka Barcelona ubingwa wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.
Alifunga
pia magoli 10 katika mechi 10 za Real iliyoishia katika hatua ya nusu fainali
ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
TUZO YA
DI STEFANO
Alikuwa
mchezaji wa kwanza kuifunga kila timu ya La Liga katika msimu mmoja, huku pia
akiwa mchezaji wa kwanza kufunga zaidi ya mabao 40 katika misimu miwili mfululizo
ya ligi hiyo.
Kiwango
chake kilitambuliwa kupitia tuzo aliyotwaa ya Trofeo Alfredo Di Stefano, ambayo
hutolewa kwa mchezaji bora wa msimu wa La Liga.
Ronaldo
pia alifuta dhana iliyojengeka dhidi yake kwamba hukosa makali katika mechi
kubwa baada ya kuonyesha kiwango cha juu na kufunga goli la ushindi la Real
Madrid dhidi ya Barcelona mwezi April na pia akang’ara katika fainali za Euro
2012.
Alifunga
mara mbili na kuipa timu ya taifa ya Ureno ushindi wa 2-0 katika mechi yao ya
mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Uholanzi, kabla hajafunga pia goli pekee
lililowapa ushindi wa 1-0 katika mechi ya robo fainali ya Euro 2012 dhidi ya
Jamhuri ya Czech.
Mchambuzi
maarufu wa soka ambaye ni Kaimu Mhariri wa mtandao wa soka wa Goal.com, Luis
Herrera, alimuelezea Ronaldo kuwa ni mchezaji ‘spesho’ aliyeipa Real ‘ubavu’ wa
kuipiku Barcelona ya sasa.
"Cristiano Ronaldo alikuwa
na msimu bora zaidi baada ya kuisaidia Real Madrid kutwaa ubingwa. Kuiuzia timu
ya Barcelona ya sasa unahitaji kuwa na mtu spesho na kwa mshambuliaji huyu
Mreno, Real wanaye mtu huyo," alisema Herrera.
TAKWIMU ZA CRISTIANO RONALDO 2011-12
|
MECHI
|
MAGOLI
|
PASI
ZA MABAO
|
|
REAL
MADRID
|
55
|
60
|
15
|
URENO
|
11
|
6
|
2
|
JUMLA
|
66
|
66
|
17
|
No comments:
Post a Comment