Kwa dau hilo mie basi... ! Kocha Alex Ferguson wa Man U |
Lucas Moura... mijihela inayolipwa na PSG imemchanganya Ferguson |
MANCHESTER,
England
KOCHA Alex
Ferguson ameelezea mshangao wake baada ya Paris Saint-Germain kuishinda Manchester
United katika mbio za kutaka kumsajili nyota wa Sao Paulo, Lucas Moura.
Kwa muda
mrefu, Man U walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kumnasa yosso huyo mwenye miaka 19,
lakini mwishowe mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil akakubali kujiunga na timu
hiyo inayosifika kwa kumwaga fedha Ufaransa kwa mkataba wa miaka minne baada ya PSG kukubali kulipa dau nono walilotajiwa
la euro milioni 45 (Sh. bilioni 86)
PSG tayari
imeshamwaga fedha nyingi kusajili wachezaji kadhaa ghali katika kipindi hiki
cha majira ya kiangazi, huku Thiago Silva, Zlatan Ibrahimovic na Ezequiel
Lavezzi wote wakikubali kutua kwenye kikosi hicho cha kocha Carlo Ancelotti
kinachopigania kutwaa taji lake la kwanza la Ligue 1, Ligi Kuu ya Ufaransa tangu
mwaka 1994 na pia kutaka kutwaa ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Ferguson anaamini
kwamba matumizi makubwa ya PSG yanaharibu mchezo wa soka, hata hivyo, akikubali
kwamba vigogo hao wa Ufaransa sasa ni wa kuchungwa sana kwani ni miongoni mwa
klabu tishio katika soka la Ulaya.
Ameiambia
tovuti rasmi ya klabu yake: "Nimeshangazwa kuona kwamba klabu inaweza
kulipa hadi euro milioni 45 (Sh. bilioni 86) ili kumsajili mvulana wa miaka 19.
"IIli
kumstua kila mmoja, ili kumfahamisha kila mtu kwamba PSG wapo, wamemsajili Thiago
Silva na Zlatan Ibrahimovic kutoka AC Milan.
"Lazima
watakuwa wameshatumia takriban paundi za England milioni 150 mwezi uliopita. Kma
mjuavyo, kikwazo pekee kwa matumizi kama hayo ni UEFA.
"Katika
masharti ya soka la Ulaya, hamtafuzu katika michuano ya Ulaya kwa kutwaa
ubingwa wa ligi au kumaliza katika nafasi ya pili, mnashiriki pale tu mnapopata
mwaliko.
No comments:
Post a Comment