Eric Abidal anavyoonekana katika siku ya utambulisho rasmi wa kikosi cha Barca 2012-13. |
Abidal akijifua |
Eric Abidal... hapa pia akijifua |
Eric Abidal akisoma Qur-an ndani ya ndege wakati yeye na wachezaji wenzake wa Ufaransa wakiwa safarini. |
Nakuombea 'jembe' letu Eric Abidal upone haraka... Lionel Messi akiwa na fulana yenye ujumbe wa kumtakia kheri Abidal. |
Abidal (wa tatu kutoka kulia)akiwa na wenzake wa kikosi kipya cha Barca 2012-13 |
Beki wa Barcelona, Eric Abidal ametangaza kuanza kujifua vikali kwa mazoezi binafsiwakati akiendelea kujiweka fiti baada ya kuendelea vizuri kiafya kufuatia upasuaji uliofanikiwa wa kumpandikizia ini jingine mwilini .
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa alifanyiowa upasuaji Aprili, na kulikuwa na hofu kwamba beki huyo wa kushoto asingerudi tena uwanjani.
Hata hivyo, Abidal amepania kucheza tena soka, na sasa ameanza kujifua vikali katika "gym" ya klabu yao na pia kufanya mazoezi binafsi akiwa mbali na wenzake wa kikosi cha kwanza.
"Enyi ndugu na marafiki zangu, natumai kwamba nyote ni wazima, nawaandikia ili kuwapa habari njema: Nimeanza tena kufanya mazoezi ya ndani, kwa siku kadhaa sasa," taarifa kupitia ukurasa wa mtandao wake rasmi wa kijamii wa Facebook ilisomeka.
Beki huyo mwenye miaka 32 alikaribishwa kwa kushangiliwa sana Jumatatu wakati wa kutambulishwa rasmi kwa kikosi cha Barcelona kabla ya mechi yao ya kirafiki ya kuwania Kombe la Joan Gamper dhidi ya Sampdoria, na Abidal alifurahishwa na upendo ulioonyeshwa kwake na mashabiki.
"Na ninapenda kuwashukuru sana wana Catalans (mashabiki wa Barca) kwa kunipokea vizuri sana kwenye Uwanja wa Camp Nou wakati wa utambulisho wetu rasmi! Nawashukuru kwa kuniunga mkono."
Katika taarifa nyingine, Eric Abidal ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu alieleza namna anavyomshukuru Mungu kwa kuendelea kumpa uzima, akisema: "Allah Akbar!"
Baada ya kusumbuliwa na kivimbe cha ini, Abidal alifanyiwa upasuaji na Aprili mwaka huu akapasuliwa tena na kupandikiziwa kipande cha ini alichopewa na binamu yake.
No comments:
Post a Comment