Monday, August 6, 2012

BOLT ASHINDA TENA DHAHABU MITA 100 OLIMPIKI

Bolt kushoto akielekea kushinda mbio za mita 100 za Olimpiki ya London 2012 usiku huu.
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (kulia) akimaliza fainali ya mbio za mita 100 katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini London Agosti 5, 2012.  Kutoka juu kuja chini: Tyson Gay wa Marekani, Mjamaica Yohan Blake, Justin Gatlin wa Marekani na Bolt. Picha: REUTERS
Chezea Bolt nyie... kijana akiwafungisha tela wapinzani wake. Picha: REUTERS
Rekodi mpya ya Olimpiki... Bolt akimaliza mbio za mita 100 na kuweka rekodi mpya ya Olimpiki. Picha: REUTERS

Mkali wao Bolt akimaliza mbio za 100 Olimpiki. Picha: REUTERS
Mlichonga sana, lakini hamniwezi.... Bolt akishangilia kwa staili yake maarufu baada ya kutetea taji lake la Olimpiki. Picha: REUTERS

Shaaa.... Nikichomoka ni kama umeme.... Bolt akishangilia baada ya kutwaa medali ya dhahabu kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini London. Picha: REUTERS

Huyu alinishinda kwenye majaribio nyumbani Jamaica akadhani anaweza, bado sana. Bolt (kushoto) akipozi na mshindi wa pili wa Olimpiki, Yohan Blake ambaye ni Mjamaica mwenzake.Picha: REUTERS
Bolt wa Jamaica (kulia) akishangilia huku akipongezwa na mshindi wa tatu Justin Gatlin wa Marekani (katikati) na mshindi wa pili Yohan Blake (kushoto)

USAIN Bolt alithibitisha kwamba kwamba yeye ndiye mwanadamu mwenye kasi kuliko wote waliopata kutokea duniani baada ya kutetea taji lake la mbio za mita 100 la Olimpiki kwa staili yake.

Bolt, ambaye alitiliwa shaka na wengi baada ya kuwa na msimu mbaya uliotokana na kubwagwa na pia kusumbuliwa na majeraha, alikimbia kwa kasi ya pili kwa ubora katika historia na kumshinda patna wake wanayefanya mazoezi pamoja Yohan Blake aliyetwaa medali ya fedha na na Mmarekani Justin Gatlin aliyetwaa ya shaba.

Muda wa Bolt wa sekunde 9.63, ambao ni sekunde 0.05 pungufu ya rekodi ya dunia ambayo ni yake mwenyewe, ulikuwa ni rekodi mpya ya Olimpiki ambayo ilishuhudia wakimbiaji saba wakitumia chini ya sekunde 10, huku majeruhi Asafa Powell pekee akishindwa kupita muda huo.

Mwanariadha huyo 25 alisema: "Niliona kwamba ningeweza kufanya jambo hili. Nilikuwa na shaka kidogo na jinsi nilivyoanza haikuwa vizuri sana duniani - lakini niliacha kuogopa, nikakomaa na ikafanya kazi.

"Nilisema kwa vitendo. Watu wanaruhusiwa kuongea - wanachoweza ni kuongea tu. Linapokuja suala la ubingwa huwa nauleta mimi."

Bolt alibwagwa na Blake katika mbio za kufuzu za Jamaica na akatumia muda wa chini zaidi aliopata kutumia katika mita 100m msimu huu.

Alipokiri kwamba majeraha ya mgongo na misuli ya nyuma ya paja vilikuwa vikimsumbua na kusema kwamba yuko fiti kwa "asilimia 95" tu, walikuwepo waliosema kwamba amekuwa mwepesi kumshinda kuliko wakati wowote tangu alipotwaa medali ya dhahabu ya Olimpiki na kuweka rekodi miaka minne iliyopita, tukio ambalo lilimjengea umaarufu alionao sasa.

Kama ushindi huu ulikuwa ni wa asilimia 95, basi rekodi yake aliyoiweka mwaka 2009 ya sekunde 9.58 huenda ingevunjwa kama angekuwa fiti kikamilifu.

Blake aliyetumia sekunde 9.75 na Gatlin (sekunde 9.79) wote waliweka rekodi zao mpya wakati Gay aliyetumia sekunde 9.80 aliishia nafasi ya nne. 


Angalia msimamo ulivyokuwa kwa ujumla:
BibAthleteMark
+ 12170 JAM BOLT Usain9.63 OR
+ 22169 JAM BLAKE Yohan9.75 =PB
+ 33216 USA GATLIN Justin9.79 PB
+ 43217 USA GAY Tyson9.80 SB
+ 53205 USA BAILEY Ryan9.88 =PB
+ 62547 NED MARTINA Churandy9.94
+ 73051 TRI THOMPSON Richard9.98
+ 82184 JAM POWELL Asafa11.99

No comments:

Post a Comment